loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watumishi 7,515 waajiriwa shule za sekondari

KATIKA kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016/2017 hadi 2018/2019 serikali imeajiri watumishi 7,515 katika shule za sekondari nchini.

Hayo yalisemwa bungeni mjini hapa jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwita Waitara alipojibu swali la Mbunge wa Masasi Mjini, Dk Rashid Chuachua (CCM).

Katika swali lake Mbunge huyo pamoja na mambo mengine alitaka kufahamu mpango wa serikali wa kupeleka kwa dharura walimu 60 wa sayansi katika shule tisa za sekondari zilizopo katika jimbo la Masasi kutokana na uhaba wa walimu wa somo hilo.

Naibu Waziri Waitara alisema kati ya watumishi hao walioajiriwa katika shule za sekondari, walimu ni 7,218 na Fundi Sanifu Maabara ni 297.

Alisema kati ya walimu walioajiriwa, wenye mahitaji maalumu ni 29, wenye elimu maalumu ni 50, walimu wa masomo ya sayansi na hisabati ni 7,089 na walimu wa lugha ni 100 ambapo walimu 15 wa sayansi walipangwa katika Halmashauri ya Mji wa Masasi.

Alisema katika mwaka wa fedha 2017/2018, shule za sekondari 1,800 zilizokamilisha ujenzi wa maabara, zilipelekewa vifaa vya maabara na kati ya hizo, sita ni za Halmashauri ya Mji wa Masasi.

Alisema vile vile katika mwaka wa fedha 2018/2019 jumla ya shule 1,258 zilizokamilisha ujenzi wa maabara zitapelekewa vifaa vya maabara na taratibu za manunuzi zinaendelea na shule tatu kati yake ni za Halmashauri ya Masasi Mji.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi