loader
Picha

Mwili wa Mugabe wawasili Harare

MWILI wa aliyekuwa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe umewasili nchini humo kutoka Singapore kwa kutumia ndege binafsi. Mugabe alikuwa Singapore akipatiwa matibabu kabla ya kufariki dunia wiki iliyopita akiwa na miaka 95.

Mugabe alikuwa rais wa pili nchini humo baada ya uhuru wa mwaka 1980. Aliongoza nchi hiyo kwa zaidi ya vipindi vinne kabla ya kuondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 2017.

Mwamba huyo wa Afrika anatarajiwa kuzikwa jumapili hii baada ya mazishi ya kiserikali yatakayofanyika jumamosi. Ndege binafsi iliyobeba mwili wa Mugabe iliwasili Harare jana saa 9:00 mchana kwa saa za nchi hiyo.

Mwili wake utawekwa kwenye Uwanja wa Rufaro mjini Mbare, Harare ambapo aliwahi kuapishwa kushika nafasi ya urais. Hata hivyo sehemu atakayozikwa haijafahamika kutokana na mvutano wa kutokubaliana kati ya familia yake na serikali ya Emmerson Mnangagwa.

WATOTO wawili wamefariki dunia, na wengine 11 wamelazwa ...

foto
Mwandishi: HARARE, Zimbabwe

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi