loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Putin afagilia maandamano

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amesema wakati mwingine maandamano ya wananchi ni jambo jema kwani yanatingisha mamlaka za juu ya nchi.

Hata hivyo amewataka vijana kuangalia zaidi masuala ya kujenga na sio kuandamana kupinga kila kitu. Rais Putin alikuwa akizungumza kwenye Mkutano wa Uchumi wa Mashariki(EEF) uliofanyika Vladivostok.

Rais Putin alitoa maoni yake hayo wakati akizungumzia maandamano makubwa yaliyotingisha mji mkuu wa nchi hiyo, Moscow na miji mingine michache hivi karibuni.

“Naamini watu wana haki ya kueleza maoni yao wakati wa maandamano. Wakati mwingine hii imeleta matokeo chanya kwa sababu yanatingisha mamlaka za nchi,”alisema.

Hata hivyo alisema ni vema maandamano hayo yakafuata sheria na kanuni na yakawa ya kujenga na si kubomoa. “Vijana wengi walioshiriki maandamano ya hivi karibuni wameonesha wana mawazo chanya, baadhi yao watakuwa wanasiasa wakubwa,”alisema Rais Putin.

Alisema waandamanaji hasa vijana wanaweza kupoteza nguvu zao kwenye mambo yasiyo na msingi badala ya kuboresha utendaji wa nchi. “Nashauri sisi wote hasa vijana tutumie nguvu zetu kwenye.

WAANDAMANAJI katika mji wa ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi