loader
Picha

Serikali yataka usindikaji uongezwe

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amewaambia wasindikaji wa korosho kuwa lengo la serikali ni kuongeza kiwango kikubwa cha usindikaji kuliko ilivyokuwa mwaka jana.

Pia, amesisitiza kuwa serikali haitanunua tena korosho bali itaweka mazingira mazuri kwa Wafanyabiashara kununua zao hilo kutoka kwa Wakulima bila ya kuwalalia.

Hasunga aliyasema hayo katika mkutano wake maaalumu alioutisha juzi katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma lengo likiwa ni kuzungumza na wasindikaji hao ili kujiandaa na msimu mpya wa ununuzi wa korosho ambapo taarifa rasmi ya Wizara itatolewa hivi karibuni.

Alisema serikali pia inaendelea na azma yake ya kuongeza thamani ya zao la korosho kwa kuwasisitiza wabanguaji kuongeza ukubwa wa mazao ya korosho kwa kusindika zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita.

“Tumeona kabla ya kutangaza taarifa rasmi ya Wizara yenye kuzindua rasmi msimu mpya wa ununuzi wa korosho, ni vyema tukutane nanyi wadau ili kujadiliana namna nzuri ya kuboresha biashara ya korosho kwa lengo la manufaa ya wakulima wetu,” alisema.

Katika hotuba yake; Waziri Hasunga alielekeza kuwa wabanguaji hao wanapaswa kutoa taarifa kwa wizara kwa msimu wa kilimo wa 2019/20 katika maeneo kadhaa ikiwemo teknolojia wanazotumia katika ubanguaji na usindikaji wa korosho.

Pia wanatakiwa kuelezea uwezo wa mashine zao kusindika kwa mwaka, idadi ya Wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda, uwezo wa viwanda kubangua na kusindika korosho kwa mwezi na kwa mwaka vilevile mapendekezo ya bei ya kununulia kabla ya msimu kuanza.

Alisema wasindikaji pia wanapaswa kuwa wa wazi katika kuishauri serikali namna nzuri ya kuboresha zoezi zima la ununuzi mpya wa korosho na kueleza changamoto wanazokutana nazo.

Awali, katika taarifa yake, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Francis Alfred alisema uzalishaji wa korosho kwa msimu huu, unatarajia kufikia tani 350,000 na kuongeza kuwa tija itaongezeka ikiwa sehemu kubwa ya uzalishaji itabanguliwa na kusindikwa hapa nchini.

 TANGU mwishoni mwa wiki iliyopita bei ya gesi inayotumika kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi