loader
Picha

BOA kufanya kazi na wadau sekta ya ujenzi

BENKI ya Afrika (BOA) tawi la Tanzania imesema itaendelea kufanya kazi na wadau wa sekta ya ujenzi nchini, kwa kuwapa huduma bora za kibenki zinazoendana na matakwa yao, ili kufanikisha miradi yao mbalimbali.

Mwaka huu, benki hiyo ilishiriki maonesho yaliyofanyika kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa sekta ya ujenzi uliokuwa na kauli mbiu “Wajibu wa wadau wa sekta ya ujenzi katika kufikia uchumi wa viwanda endelevu kwa ustawi wa jamii”. Mkutano na maonesho hayo vilifanyika Dar es Salaam.

Akizungumzia huduma za kibenki zinazowalenga wadau wa sekta ya ujenzi, Meneja wa Huduma wa benki hiyo kwa Tanzania, Maxmillian Mwita alisema BOA hutoa huduma rafiki kwa wadau wa sekta hiyo, ambazo ni pamoja na huduma ya dhamana ya zabuni na mkopo wa kununua vitendea kazi.

“BOA -Tanzania kama benki ya kimataifa ina huduma mbalimbali kwa wafanyabiashara wa sekta ikiwemo wa sekta ya ujenzi na iko tayari kuwahudumia wote kufanikisha kazi zao hususani wale wanaokidhi vigezo vyetu”, alisema.

Akifafanua kuhusu huduma hizo, alisema kuna huduma ijulikanayo kama ‘letters of credit’, ambapo benki hiyo hutoa dhamana kwa wateja wa benki ili kuweza kupata vifaa vya ujenzi kutoka kwa wazalishaji na kulipia baada ya kuridhishwa na mzigo.

Huduma nyingine iliyolenga kuwainua wadau wa sekta ya ujenzi ni huduma ya kutoa dhamana wakati wa kushindania zabuni, ambayo inathibitisha kuwa wakipata zabuni, benki itatoa fedha za kuendesha mradi, hata kabla ya kupokea malipo ya kazi.

Mwita alisema pia kuwa benki ina huduma ya kuwezesha kununua vitendea kazi ambapo kwa wadau wa sekta ya ujenzi ambao ni wateja wa benki, huwezeshwa kununua vifaa vya kuendesha miradi yao ya ujenzi, kama magari na mitambo.

Alisema BOA-Tanzania imejipanga kwenda sambamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo kwa kiasi kikubwa imefanikisha miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu na majengo.

“Tumejipanga kuhakikisha tunatoa huduma za kufanikisha miradi ya ujenzi kwa wateja wetu wanaokidhi vigezo,”alisisitiza Mwita.

KATIBU Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi