loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwakyembe ahamasisha kujifunza ukalimani

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, ametoa rai kwa jamii nchini kujifunza ukalimani kwa lengo la kujijengea mazingira mazuri ya kupata ajira ndani na nje ya nchi.

Akizungumza juzi wakati wa mahafali ya shule za Bethel Mission za jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe alisema licha ya taaluma ya ukalimani kuwa na soko zuri la ajira, bado kuna idadi ndogo ya wataalamu wa fani hiyo na hivyo kuiasa jamii kuichangamkia kwa haraka.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, takwimu alizonazo kuna idadi ndogo ya wakalimani waliopo nchini ikiwa ni tofauti na mahitaji yaliyopo na hivyo kusababisha changamoto kwa baadhi ya taasisi au ofisi zinazowahitaji.

“Kwa kumbukumbu nilizonazo wakalimani waliopo kwa sasa nchini idadi yao hawazidi 20, na hivyo kuonyesha kuwa bado kuna kiwango kikubwa cha watu wenye fani hiyo wanaohitajika ili kukidhi mahitaji,” alisema Mwakyembe.

Rai hiyo ya Mwakyembe aliitoa baada ya kukoshwa na vipaji vya watoto wawili ambao ni wahitimu wa mahafali hayo kwa kipaji chao cha kuigiza kazi ya uchungaji huku mmoja akitafsiri kwa Kiswahili, hatua ilimfanya kuupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuwalea watoto hao kinidhamu na kiroho.

Aidha, Waziri Mwakyembe aliwaasa wazazi kuendelea kuwalea watoto wao katika maadili mema kama ambavyo shule hiyo imekuwa ikifanya kwa madai kuwa kufanya hivyo kutasaidia kujenga taifa la watu waadilifu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shule hiyo ya Bethel Mission Emmanuel Mshana alisema mbali na shule hiyo kujivunia kwa matokeo mazuri kwa wanafunzi katika mitihani ya kitaifa, pia wamekuwa wakiwajengea nidhamu bora kwa wanafunzi hao ili kuwa na kizazi bora.

Alisema hiyo imekuwa na ushirikiano wa karibu na wazazi ili kuhakikisha wanafunzi wanaosoma katika shule hizo wanahitimu wakiwa na ufaulu mzuri na kuwafanya waweze kupata nafasi za kuendelea na ngazi za juu katika masomo yao.

Alisema mikakati ya baadaye ya shule hiyo ni kujenga shule zake za sekondari ili kuwawezesha kuwaendeleza kimasomo wanafunzi wanaoanza nao kuanzia ngazi ya shule za msingi na awali.

Pia, Mshana alisema katika kuwarahisishia wazazi katika suala zima la ulipaji wa ada za masomo kwa watoto wao, shule hiyo imeweka utaratibu unaomuwezesha mzazi kulipa kwa awamu nane tofauti, lengo ni kumpunguzia mzigo unaotokana na ukali wa maisha.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi