loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kushawishi rushwa kwampandisha kizimbani

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Ilala imemfi kisha mahakamani Meneja wa kampuni ya Shahi Engineering and Construction Limited, Angrej Singh, ikimtuhumu kushawishi kutoa rushwa kwa Ofi sa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mkuu wa Takukuru Ilala, Christopher Myava, alisema Singh alifanya hivyo ili asamehewe riba na adhabu aliyopaswa kulipa serikalini.

Alidai kampuni hiyo ilipaswa kulipa zaidi ya Sh milioni 80, lakini Singh hakutaka kulipa deni hilo, badala yake alishawishi atoe rushwa ya Sh milioni tano, jambo ambalo lingesababisha kupotea kwa mapato ya serikali.

Alidai kuwa mtuhumiwa huyo akiwa katika maeneo ya mgahawa wa Mary Brown mtaa wa Mrima na Jamhuri wilayani Ilala, Dar es salaam, Agosti 06, mwaka huu, alimshawishi Ofisa Forodha wa TRA, Mkabakuli ili ampe rushwa hiyo.

Alisema mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani Agosti 10, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam kujibu shitaka lake. Wakati huo huo, alisema Takukuru imejipanga kudhibiti rushwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kuanzia ngazi za chini.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Mussa Dotto na Lovini Kefa, Tudarco

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi