loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TADB- Njooni tuwape fedha za miradi

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imesema, silaha yao kubwa ni uwezo wa kutoa mikopo ya muda mrefu.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Japhet Justine amesema jijini Dar es Salaam kuwa, wanataka kuonyesha tofauti kati ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo na benki ya kibiashara.

“Ukienda kwenye benki ya biashara mtaji wa kukuvumilia atakubana miaka minne, zaidi miaka mitano, sisi tunakwenda mpaka miaka kumi, mpaka 12, mpaka 15 kwa hiyo inategemea na aina ya mradi” amesema Justine.

Ameyasema hayo Dar es Salaam wakati menejimenti ya TADB ikizungumza na ujumbe wa uongozi wa mkoa wa Pwani akiwemo Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Evarist Ndikilo na timu ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

“Sisi uwezo wetu mkubwa ni kwenye kutengeneza miradi ya muda mrefu kwa hiyo kuanzia umwagiliaji lakini pia kutengeneza miundombinu ya utunzaji wa vyakula ambao inaweza ikawa ni maghala au vihenge vya kisasa”amesema.

Amesema TADB ina uwezo mkubwa wa kufadhili miradi, na kwamba ,fedha zao wanaziita ni mitaji ya kuvumilia Ametaja miradi ambayo wapo tayari kuigharamia kuwa ni ujenzi wa viwanda vya kubangua korosho mkoani Pwani.

“Yule anayetaka kuweka kiwanda sisi tutakuwa tayari kumsikiliza na kuona tunawezaje kutengeneza na kuhakikisha hii tani 22, 168 ibanguliwe ndani”amesema Justine.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, ametoa ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi