loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri Mkuu aonya wafanyabiashara

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatahadharisha wachuuzi wa mazao ya kilimo wanaokiuka maelekezo ya serikali kwa kuendelea kutumia mfumo ‘rumbesa’ badala vipimo vilivyoidhinishwa.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo bungeni, Dodoma (Septemba 12, 2019) katika kipindi cha maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu wakati  akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mlalo, Abdallah Shangazi  aliyeuliza endapo serikali ipo tayari kufanya operesheni ya kudhibiti tatizo hilo linalozidi kuwafukarisha wakulima.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu amekiri uwepo wa wafanyabiashara wengi wa mazao nchini kutofuata sheria na taratibu zilizowekwa na serikali katika kutumia vipimo vilivyoidhinishwa na mamlaka zinazohusika.

“Serikali imeweka utaratibu wa mazao yote yanayolimwa na kuingia kwenye masoko lazima masoko hayo yatumie vipimo halisi ili viweze kulipa bei stahiki na mkulima aweze kunufaika.

“Nirudie tena kutoa wito kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi, maafisa kilimo  pamoja na maafisa ushirika kwenye maeneo yao wasimamei biashara hii na kufanya operesheni kwenye maeneo yote ya masoko ili kujiridhisha kwamba mazao yetu yananunuliwa kwenye vipimo ambavyo vimekubalika huu ndio msisitizo wa serikali na tutaendelea kuusisitiza,” amesema Waziri Mkuu.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo bungeni na kuwaagiza wanunuzi wa mazao kuacha kuwapangia bei wakulima huku akiwataka wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, maafisa kilimo  pamoja na maafisa ushirika kusimamia maslahi ya wakulima.

Ununuzi wa mazao kwa kujaza kupita kiasi kwenye vibebeo, rumbesa, unaelezwa kuwa unaathiri wakulima kwa kuwanyonya.

Kutokana na hali hiyo, mnamo Septemba 2, 2019, kupitia kituo cha luninga cha ITV, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alikiri kuhusu uwepo wa malalamiko ya wakulima mkoani humo kulazimishwa kutumia vipimo vya rumbesa na wanunuzi wa vitunguu katika eneo la Mang’ola alisema kuwa suala hilo litatatuliwa endapo wananchi wenyewe watakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka zinazohusika kudhibiti hali hiyo.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Na Ombeni Utembele

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi