loader
Picha

Mbowe, wenzake 8 wana kesi ya kujibu

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake wanane wa kesi ya kujibu mashitaka ya uchochezi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imesema leo.

Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama hiyo Thomas Simba amesema, upande wa mashataka kwa kuzingatia mashuhuda wanane umeona washitakiwa hao wanapaswa kujibu mashitaka yanayowakabili.

Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Chadema Vicent Mashinji, na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar Salum Mwalimu.

Wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya, na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko.

Wanatakiwa kujibu mashitaka 11 ya kula njama kufanya makosa, kukusanyika isivyo halali, kufanya vurugu, uchochezi na nia mbaya ya kufanya makosa.

Wanadaiwa kufanya makosa hayo kati ya Februari Mosi hadi 16 mwaka jana jijini Dar es Salaam.

WATOTO yatima na wanaoishi kwenye mazingira wa magumu wa shule ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi