loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Raia wa nje marufuku kuasili mtoto Kenya

Serikali ya Kenya imepiga marufuku raia wa nchi nyingine kuasili watoto nchini humo.

Marufuku hiyo imetangazwa leo baada ya kikao maalumu cha Baraza la Mawaziri nchini humo, kilichoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na kuhudhuriwa pia na Naibu Rais, William Ruto.

Kutokana na tamko hilo, shughuli zote za kuasili watoto zinazofanywa na Taasisi ya Ustawi wa Jamii zimesitishwa.

Wizara ya Kazi na Usimamizi wa Jamii nchini humo imeagizwa kuandaa sera mpya itakayoongoza mchakato wa kuasili watoto nchini humo.

Tamko hili limetolwa zikiwa zimepita wiki mbili baada ya kituo cha televisheni nchini humo kuonyesha mateso wanayopata watoto kwenye makazi maalumu ya watoto yaliyo chini ya ustawi wa jamii.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi