loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barabara Singida -Tanga kujengwa kwa awamu

SERIKALI itajenga kwa awamu, barabara inayounganisha mkoa wa Singida na Tanga yenye urefu wa kilometa 461 ili kuhakikisha wananchi wa maeneo inakopita wanapata maendeleo ya kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (CCM).

Mtaturu alisema yupo imara kuwawakilisha wananchi wake na akataka kujua barabara kutoka Njiapanda-Mwakuingu-Kwamtoro hadi Handeni iliyofanyiwa upembuzi yakinifu muda mrefu, lini sasa itaanza kujengwa ili kusaidia wananchi wa Ikungi na mkoa wa Singida kupata maendeleo.

Akijibu swali hilo, Waziri Kwandikwa alisema barabara ya Njiapanda- Makiungu- Mtoro-Chemba hadi Handeni yenye urefu wa kilometa 461 usanifu wake umekamilika na itaanzwa kujengwa hatua kwa hatua ili kuwanufaisha wananchi wa eneo hilo.

Katika swali la Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Allan Kiula alihoji serikali itajenga lini barabara ya lami inayounganisha Mkoa wa Simiyu na Singida kupitia daraja la Sibiti lililopo Wilaya ya Mkalama.

Akiuliza swali bungeni jana, Mbunge huyo alisema Sera ya Serikali ya awamu ya tano ni kuunganisha barabara za lami kati ya mkoa na mkoa. “Je, lini serikali itajenga barabara ya lami inayounganisha mkoa wa Simiyu na Singida kwa kupitia daraja la Sibiti," amehoji.

Waziri alisema mikoa ya Simiyu na Singida inaunganishwa na barabara ya Gumanga hadi Singida mjini yenye urefu wa kilomita 341 na inaunganishwa pia na barabara ya kutoka Bariadi kupitia Kisesa hadi Singida mjini.

Alisema barabara hiyo ina urefu wa kilometa 338 na barabara hizo zinahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).

Alisema ujenzi wa daraja la mto Sibiti lenye urefu wa mita 82 umekamilika na ujenzi wa barabara unganishi za kilometa 25 umekamilika kwa kiwango cha changarawe ambapo manunuzi ya kuzijenga kwa lami yanaendelea.

"Barabara ya Sibiti hadi Iguguno yenye kilometa 106 ipo upande wa mkoa wa Singida na sehemu ya barabara hii kuanzia Sibiti hadi Mkalama kilometa 27 inaendelea kufanyiwa usanifu wa awali kupitia mradi wa Sengereti Southern Bypas na sehemu iliyobaki ya barabara hii ni barabara ya kiwango cha Changarawe na hupitika majira yote ya mwaka,"amesema.

Amesema upande wa Simiyu, barabara ya kuanzia Sibiti hadi Ng'oboko kupitia Lalago-Maswa hadi Bariadi, sehemu ya kuanzia Bariadi hadi Maswa yenye urefu wa kilometa 49.5 inaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.

Aidha, amesema, sehemu ya kuanzia Maswa hadi Sibiti kilometa 146.83 inaendelea kufanyiwa usanifu wa awali kupitia mradi wa Serengeti Southern Bypass barabara inayoanzia Ng'hoboko kupitia Kisesa hadi Bariadi ni barabara ya changarawe na inapitika majira yote ya mwaka.

"Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hii inaendea kutafuta fedha kufanya usanifu wa kina sehemu nyingine zilizobaki ili kujengwa kwa lami," alisema.

MASHIRIKA mbalimbali ya kimataifa ya usafiri ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi