loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benki yalipa bil 2.4/- fidia bima ya amana

BENKI ya FBME Ltd ipo katika hatua za ufilisi na hivyo haiendeshi shughuli za kibenki nchini.

Hadi kufikia Septemba 9, mwaka huu, jumla ya kiasi cha Sh milioni 2,404.2 kimelipwa kwa wateja 3,426 kama fidia ya bima ya amana.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi (CCM), Jaku Hashim Ayub.

Katika swali lake, Mbunge huyo alihoji ni lini Benki hiyo italipa wateja amana zao.

"Je, benki iko katika hali gani sasa? Na je, Benki Kuu ya Tanzania ina dhamana gani katika kulinda mabenki? amehoji.

Alisema kiasi hicho cha fedha ni sawa na asilimia 55.9 ya kiasi chote kilichotarajiwa kulipwa kama fidia ya bima ya amana kwa wateja wote 6,628 waliopo Tanzania pamoja na wateja waliopo nje ya Tanzania.

"Aidha, Sh milioni 2,401.2 zimelipwa ikiwa ni asilimia 83.3 ya lengo la kulipa Sh milioni 2,882.6 kwa wateja waliopo Tanzania tu,"alisema.

Hata hivyo, amesema wateja waliokuwa na amana zaidi ya Sh milioni 1.5 watalipwa kiasi kilichobaki kwa mujibu wa sheria na taratibu za ufilisi.

"Kiasi kitakacholipwa kwa wenye amana zaidi ya Sh milioni 1.5 kitategemea fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo ya mali za benki pamoja na ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wadeni wa benki hiyo," alisema.

Awali, alifafanua kuwa benki hiyo ilifutiwa leseni ya kufanya biashara hapa Tanzania na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mei 8, mwaka 2017 kwa tuhuma za kujihusisha na utakatishaji fedha huko nchini Marekani.

"Pia BoT iliteua Bodi ya Bima ya Amana kuwa mfilisi wa benki hiyo katika kutimiza wajibu wake wa msingi, Bodi ya Bima ya amana ilianza kulipa fidia kwa mujibu wa sheria kwa waliokuwa na amana katika benki hiyo kuanzia Novemba 2017 na bado inaendelea," alisema.

Alisema, Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 imeipa BoT mamlaka kutoa leseni, kutunga kanuni, kusimamia benki zote zinazochukua amana za wateja na kuchukua hatua za kisheria kwa benki zinazoendesha biashara bila kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.

" Benki kuu imepewa mamlaka ya kusimamia na kudhibiti benki na taasisi za fedha ili kuhakikisha amana za wateja zinakuwa salama na kuna usalama, utulivu na udhibiti wa sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla,"alisema.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, ametoa ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi