loader
Picha

Ujerumani yatoa bil 26/- miradi ya afya Tanzania

SERIKALI ya Tanzania imesaini mkataba wa makubaliano na Serikali ya Ujerumani wa kutekeleza mradi katika sekta ya afya nchini utakaogharimu Sh bilioni 26.6

Akizungumza jana mara baada ya kusaini makubaliano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Zainab Chaula alisema mkataba huo ni wa tano na unatekelezwa kila baada ya miaka mitatu.

Amesema mkataba huo umejikita katika kuimarisha sekta ya afya nchini katika maeneo manne ambayo ni kuimarisha afya ya msingi ngazi ya halmashauri katika zahanati na vituo vya afya.

Dk Chaula amesema mkataba pia umelenga katika uimarishaji wa taarifa za afya, kuimarisha afya ya mama na mtoto, uzazi wa mpango, bima ya afya kwa wajawazito na utawala bora.

Akizungumzia utekelezaji wa mkataba huo, Dk Chaula alisema: " Huu ni mkataba wa tano ulioanza tangu 2003 na umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka mitatu, Mkataba wa sasa umejikita katika maeneo manne ambayo ni kuimarisha afya ya msingi ngazi ya halmashauri katika zahanati na vituo vya afya, uimarishaji wa taarifa zetu, kuimarisha afya ya mama na mtoto, uzazi wa mpango na bima kwa wajawazito na utawala bora,” amesema.

Akifafanua zaidi, Dk Chaula amesema katika suala la utawala bora linalenga namna ya kuzitumia fedha hizo kulingana kanuni na taratibu za nje.

Amesema katika kutekeleza miradi iliyopo chini ya mkataba huo, wamekubaliana na wahisani kutumia mfumo wa 'Force Account' ambao uliweza kuleta mafanikio makubwa ya ujenzi wa vituo vya afya nchini, badala ya kutumia wakandarasi kama ilivyokuwa kwenye miradi ya awali.

Alisema kuwa hadi sasa kuna vituo vya kutolea huduma za afya vipatavyo 470 katika ngazi ya zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya ambavyo vimejengwa na kuboreshwa.

Dk Chaula amesema pia serikali imewekeza takribani Sh bilioni 100.5 kwa ajili ya kujenga Hospitali za Wilaya 67 katika wilaya ambazo hazikuwa na hopsitali ya wilaya.

"Kwa sasa katika sekta ya afya tunafanya vizuri, maana wajawazito wanaokwenda kujifungulia vituo vya afya inakaribia kuwa asilimia 80, tumeimarisha sana utoaji wa huduma za afya,"alisema.

Rais John Magufuli amepokea hati ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi