loader
Picha

Mugabe kuzikwa na serikali, familia yaridhia

Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe utazikwa kwenye eneo la makaburi ya viongozi wa taifa hilo, jijini Harare, siku ya Jumapili Septemba 15, 2019.

Hii ni baada ya familia ya kiongozi huyo kufikia muafaka na serikali ya nchi hiyo kuhusiana na wapi azikwe Mugabe.

Akizungumza baada ya muafaka huo, msemaji wa familia Leo Mugabe akizungumza na kituo cha televisheni cha Zimpapers asubuhi ya leo, Ijumaa, amesema familia na wazee wa kimila wamekubali ombi la serikali kushughulikia mazishi.

“Nachukua nafasi hii kukanusha uvumi kuwa wazee wa mila wamelipwa ili kufanya maamuzi hayo, hakuna aliyelipwa kufanya maamuzi haya,” ameeleza.

KILA mmoja ana njia yake ya kuonesha heshima ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi