loader
Picha

DC: Changamkieni mikopo ya biashara

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ametoa wito kwa wafanyabishara jijini humu kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na taasisi za kifedha ili wazitumie kukuza mitaji yao ya kibiashara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa hafla ya jioni ya Uzinduzi wa Klabu ya wafanyabiashara ya Benki ya NBC ya mkoa wa Dodoma, Mkurugenzi wa jiji hilo,Godwin Kunambi alisema mbali na kuipongeza benki hiyo kwa mabadiliko makubwa ya kihuduma, ipo haja ya makusudi kwa wafanyabiashara wa jiji hili kuitumia vema benki hiyo kupata nguvu ya kiuchumi.

“Dodoma kwasasa kuna utekelezaji wa miradi mikubwa mingi ikiwemo barabara, stendi ya mabasi ambayo ni kubwa zaidi Afrika Mashariki, upanuzi wa uwanja wa ndege, ujenzi wa viwanja vya mapumziko vitachochea mzunguko mkubwa wa fedha na ongezeko la watu.

“...Ni fursa kwa wafanyabiashara kushirikiana vema na benki kama NBC ili kukuza mitaji itayowawezesha kufanya uwekezaji utakaowanufaisha na mabadiliko hayo”, alibainisha.

Alitolea mfano umuhimu wa wafanyabiashara hao kuwekeza kwenye sekta ya usafiri ambapo kwasasa serikali jijini humu ipo kwenye mpango wa kuondoa magari madogo ya abiria, maarufu kama vipanya kwenye mizunguko ya mjini, ili kutoa fursa kwa magari makubwa kufanya kazi hiyo.

Akizungumza kuhusu uanzishwaji wa Klabu hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kati na Wadogo wa benki ya NBC, Evance Luhimbo alisema pamoja na mambo mengine, klabu hizo zinalenga kutoa mafunzo kwa wateja wa benki hiyo kuelewa mabadiliko ya uboreshwaji wa huduma zinazoihusu.

Alisema katika kufanikisha hilo wanawaku tanisha pamoja wajadili fursa za kibiashara sambamba na kuwajengea uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya kibiashara ikiwemo masuala ya kodi na taratibu za kijiunga na taasisi wadau biashara ili ziwasaidie.

“Benki ya NBC kwasasa ipo kwenye mabadiliko makubwa ya kihuduma kwa wateja ndio maana tunawaweka karibu. Mbali na benki kuwajengea uelewa kama huduma zetu na taasisi wadau ikiwemo Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA)na Baraza la Uwezeshaji (NEEC)na nyingine nyingi”.

“Pia, tumekuwa tukipokea maoni kutoka kwa wateja wetu yanayotuwezesha kubuni huduma zinazoendana na uhalisia wa mahitaji yao ya kifedha”, alisema.

Awali, wakiwasilisha mada kwenye kongamano la uzinduzi wa Klabu hiyo muwakilishi wa TCCIA, Patrick Magai na muwakilishi wa NEEC, Nyakao Mturi walitoa wito kwa wafanyabiashara wadogo kuunganisha nguvu ya kimitaji ili wapate nguvu ya pamoja itakayowawezesha kushiriki fursa kubwa za kibiashara ndani na nje ya nchi.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi