loader
Picha

TARI kushiriki kuhakikisha uchumi viwanda

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Utafi ti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dk, Geoffrey Mkamilo amesema taasisi hiyo itaendelea kufanya utafi ti, kusimamia shughuli za kilimo na kuhamasisha wadau kutumia teknolojia bora za kilimo ili kufi kia uchumi wa viwanda ifi kapo 2025.

Dk Mkamilo alisema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na HabariLeo baada ya kumaliza mkutano wa wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema katika mkutano huo lilijadiliwa suala la ubora katika bidhaa hivyo ubora huo unaanzia shambani kwani taasisi hiyo inafanya utafiti unaolenga msoko mbalimbali ya nafaka nchini.

“Sasa hivi uzalishaji si mkubwa, ilikuongeza uzalishaji lazima uanzie shambani ambapo huko kunahitajika teknolojia za kisasa pamoja na mbegu bora, Tari ndiyo sehemu yake”alisema.

Alisema Tari ipo kwa ajili ya kutoa teknolojia mbalimbali zinazoleta majibu chanya kwa ajili ya kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii.

Alisema kwa kuwa taasisi hiyo inajihusisha na usambazaji wa teknolojia katika kuwafikia wakulima na wadau wengine wa kilimo, inapaswa uzalishaji uwe mzuri kwa kuwa wakulima watatumia teknolojia bora za kilimo ikiwemo mbegu za kisasa.

Aliwataka wadau wa kilimo kuvitumia vituo vya kilimo zaidi ya 15 vilivyopo nchini kwa sababu ni kati ya hivyo kila kimoja kina jukumu la kitaifa la kufanya utafiti na maendeleo ya zao moja au zaidi ya moja.

Katika mkutano huo, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema Tanzania ina eneo linalofaa kwa kilimo linalokadiriwa kuwa hekta 44 milioni, Kati ya hizo, hekta milioni 29.4 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi