loader
Picha

Taasisi ya MOI yahimiza kutokimbilia matibabu nje

TAASISI ya Mifupa Muhimbili (MOI) imetaka wananchi kutumia fursa za huduma zake kupunguza gharama za matibabu nje ya nchi.

Kaimu Mkuu kitengo cha Uhusiano cha MOI, Patrick Mvungi alisema jana serikali imewekeza kwa kuboresha huduma katika hospitali hiyo hatua ambayo wananchi wanapaswa kutumia fursa hiyo kutibiwa nchini.

“Awali wananchi wengi walilazimika kwenda nje ya nchi kupata matibabu zaidi ya upasuaji wa mifupa, ubongo, uti wa mgongo na mengine katika nchi kama vile India na kwingineko lakini huduma hizi zimeboreshwa hapa kwetu sasa na zinapatikana,”alisema Mvungi.

Alisema baada ya kuwezeshwa na serikali kupanua miundombinu na ununuzi wa vifaa tiba, taasisi imepanua wigo la huduma kwa kuongeza huduma za upasuaji kama wa goti na bega kwa njia ya matundu, upasuaji wa mgongo kwa kufungua eneo dogo.

Huduma nyingine zinazotolewa ni upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo kupitia tundu la pua, kunyoosha viungo kwa watoto, kuzibua vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo, upasuaji wa mfupa wa kiuno pamoja na upasuaji mkubwa na mdogo wa ubongo.

Mvungi alisema MOI ina gharama nafuu za upasuaji ikilinganishwa na hospitali nyingine za nje ya nchi. Alitoa mfano wa upasuaji unaotolewa na taasisi hiyo kwa bei nafuu ni pamoja na wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo ambao unagharimu takribani Sh milioni 10 ikilinganishwa na Sh milioni 60 zinazotozwa nchini India.

Oktoba 29,2015, Raisi John Magufuli alifanya ziara katika taasisi hiyo pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kujionea changamoto mbalimbali za huduma ya tiba. Aliahidi kufanya maboresho yanayoendelea MOI.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Denis Dominick, Tudarco

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi