loader
Picha

Uhusiano na China wanufaisha UDSM

UHUSIANO mzuri kati ya China na Tanzania umetajwa kuleta manufaa kielimu kutokana na kuwezesha wahadhiri na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kubadilishana uzoefu katika elimu.

Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye amesema Profesa Anangisye alisema hayo wakati akizindua warsha iliyoandaliwa na chuo kupitia Taasisi ya Confucius pamoja na idara ya Historia, kuhusu ushirikiano wa China na Tanzania.

Alisema kupitia ushirikiano huo wa kihistoria kwa nchi hizi, China imekuwa ikitoa nafasi kwa wahadhiri na wanafunzi wa UDSM kwenda kusoma kwenye vyuo vyao katika fani mbalimbali.

“Tuna uhusiano katika masuala ya historia, hapa chuoni kuna kituo cha historia cha kimataifa. Mahala popote kunapokuwa na mabadilishano ya mawazo kwa wanafunzi wanapata vitu vipya katika kibadilishana ujuzi,” alisema Profesa Anangisye.

Mkurugenzi katika Taasisi ya Confucius chuoni hapo, Profesa Aldian Mutembei alisema idara ya historia ya UDSM imeandaa majadiliano yatakayoelezea maendeleo yaliyopo.

“China kwa sasa imepiga hatua kubwa katika maendeleo inabidi kuangalia ni wapi kama Tanzania tulikosea ili kuwa sawa kwani miaka ya 60 nchi hizi mbili zilikuwa sawa kiuchumi,” alisema.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi