loader
Picha

Swedi Nkwabi ang’atuka Simba

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa klabu ya Simba kwa upande wa wanachama wa klabu hiyo, Swedi Mkwabi amejiuzulu nafasi hiyo ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kuchaguliwa bila kupingwa Katika barua aliyotuma kwa klabu hiyo, Nkwabi amesema kuwa ameamua kujuzulu nafasi hiyo ili aweze kupata muda mwingi zaidi wa kufanya shuguli zake binafsi.

Klabu ya Simba kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram umemtakia Nkwambi kila la kheri kwenye shughuli zake binafsi, jambo linalithibitisha pasi na shaka kuwa Wekundu hao wameipokea barua ya Nkwabi.

Ikumbukwe kuwa Nkwabi alichukua nafasi ya uenyekiti kupitia uchaguzi ulifanyika Novemba, mwaka jana ambapo alipita bila kupingwa baada ya mpinzani wake kujitoa kwenye dakika za mwisho

NBA iko kwenye mazungumzo ya kuanza tena msimu kwenye hoteli ...

foto
Mwandishi: Bosha Nyanje

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi