loader
Picha

Kampuni yazindua huduma kuunganisha wafanyabiashara

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo imezindua huduma mpya itakayowezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini kuwa pamoja kibiashara.

Huduma hiyo ya ‘Office internet’ ilizinduliwa jana jijini Dar es Salaam kupitia kitengo cha biashara cha kampuni. Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Pavan Ramadhani aliwaambia waandishi wa habari kuwa huduma ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na programu za Microsoft Excel, Power Point na Outloot.

Alisema mfumo una uwezo wa kuunganisha zaidi ya wafanyabiashara 32 ambao wataweza kubadilishana mawazo kwa pamoja, kufanya mkutano wa pamoja kwa njia ya video kwenye simu, kuhariri kazi moja kwa pamoja na kupangiana mikakati ya kazi.

Alisema ili mtu aweze kupata huduma hiyo, lazima aingie mkataba na kampuni kwa muda usiopungua miaka miwili kabla ya kukabidhiwa kifaa kitakachoweza kuunganishwa apate huduma husika.

“Tulifanya kazi kwa ushirikiano wa karibu sana na wateja wetu, ambao walituonesha maeneo matatu muhimu yenye changamoto, kwanza kuunganisha huduma ya intaneti ya kasi, ukosefu wa maana halisi ya matumizi ya intaneti na mwisho uhusiano na biashara,” alisema.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Mohamed Mussa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi