loader
Picha

Bunge Mtandao kuwa msaada mkubwa kwa wabunge

BUNGE Mtandao (BM) litaokoa takribani Sh milioni 13.5 zilizokuwa zikitumiwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kuchapisha karatasi zinazotumika kila siku katika vikao 88 katika mikutano minne kwa mwaka.

Akizungumza kabla ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzindua rasmi Bunge Mtandao mwishoni mwa wiki jijini hapa, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema katika kila kikao huchapishwa nakala 600 za karatasi sawa na karatasi 52,800 kwa vikao 88.

Alisema Bunge Mtandao ni msaada mkubwa kwa wabunge wenye simu zenye android kwani wakisika na kupakua watapata habari za Bunge wakati wote kuliko ilivyo sasa ambapo wanapata habari nyingi wakati wa vikao tu.

Alisema Bunge hilo ndilo limechelewa kuingia katika mawasiliano ya kidigitali na kuachana kutumia karatasi katika mabunge ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda na Rwanda ambazo ziliacha kutumia karatasi siku nyingi.

Alisema hata katika Mkutano wa Mabunge ya Afrika (PAC) yaliyofanyika Zanzibar, walikubaliana kuachana ma mfumo wa kutumia karatasi na kuweka msukumo katika kutumia mawasiliano ya kidigitali.

Alisema wameanza na karatasi hizo (order paper), lakini watahakikisha Bunge lijalo mawasiliano yote baina ya wabunge na Bunge yanafanyika kupitia simu badala ya kujaza makaratasi katika meza za wabunge.

Akizindua Bunge Mtandao, Waziri Mkuu Majaliwa alisema safari ya uendeshaji Bunge Kidigatali imeanzia hapo kwa kuondoa makaratasi ya shughuli za kila siku za Bunge na itaendelea.

Alisema uzinduzi wa Bunge Mtandao utachangia maendeleo ya matumizi ya Tehama katika mawasiliano ya taasisi hiyo na hasa katika kupeana taarifa muhimu ndani ya Bunge.

Waziri Mkuu alisema kwa Bunge kuingia katika mfumo huo, ni kuunga mkono juhudi za serikali ambayo ilianza kutumia mfumo katika masuala mawasiliano na ukusanyaji wa maduhuli, kodi na hata kufanya miamala.

Akitoa neno la shukrani, mbunge mzoefu kwa miaka 25 akiwa bungeni, Richard Ndassa alisema kitendo cha Bunge kupata taarifa kupitia simu za viganjani ni hatua kubwa.

Ndasa ambaye ni Mbunge wa Sumve mkoani Mwanza, alisema kwa uzoefu wake miaka 25 bungeni pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, miaka ya 1990 mbunge alihitaji gari dogo kusafirisha makabrasha mbalimbali aliyokusanya bungeni katika vikao kwa mwaka.

Ndasa alimkumbusha Spika wa Bunge, Ndugai kukumbuka ahadi yake ya kuwanunulia wabunge (Ipad) kwa ajili ya kupata habari za Bunge kupitia vifaa hivyo.

Mtalaamu wa Tehama Bungeni, Lily Mraba alisema mtumiaji wa Bunge Mtandao atapata taarifa kwa haraka kupitia simu yake kutokana na urahisi wa kutumia mtandao huo na wengi zaidi.

Alisema takwimu zinaonesha asilimia 86 ya watu duniani wanaotumia mitandao wanatumia simu wakati wanaobaki asilimia 14 tu ndio wanatumia tovuti au njia nyingine katika kupata habari.

Alisema takwimu nyingine zinaonesha watumiaji wa mitandao ya mawasiliano asilimia 67 wanatumia simu zaidi na asilimia 33 wanatumia kompyuta za mezani hivyo, ni rahisi kwa wabunge kupakua habari kupitia Bunge Mtandao kupitia simu zao.

“Wabunge wataweza kupata picha, sheria, miswada, orodha ya shughuli za Bunge zitapatikana kwa kupakua Bunge Mtandao kupitia simu zao kila wakati,” alisema Mraba.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Na Magnus Mahenge, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi