loader
Picha

Nane washikiliwa ugomvi wa mashamba

POLISI mkoani Mbeya inawashikilia watu nane kwa tuhuma za kujeruhi katika vurugu zilizojitokeza kutokana na mgogoro wa kugombea mashamba wilayani Mbarali.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Kerome Ngowi wanaoshikiliwa ni wakazi wa Kata ya Ubaruku wilayani Mbarali, Denis Segele (36), Kapilipili Sichura (35) na Nebati Tulyanje (30).

Wengine ni wakazi wa Kijiji cha Msesule, Jumanne Mashaka (52), Kasuka Bulhama (56) na Arnold Kibodi (15), mkazi wa Mabadaga Amos Kita (56) na mkazi wa Makondeko, Edward Mbangala (37).

Ngowi alisema Septemba 11, mwaka huu saa nne asubuhi katika Kijiji cha Msesule, Kata ya Mapogoro Tarafa ya Rujewa kundi dogo la wakulima katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mahalala wakiwa shambani kwao wanasafisha mfereji wa umwagiliaji maji, walivamiwa na wananchi wa Kijiji cha Msesule wakiongozwa na watu wawili ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi.

Alisema miongoni mwa watuhumiwa hao ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Msesule ambaye anaendelea kutafutwa baada ya kukimbilia kusikojulikana baada ya kushiriki kwenye tukio hilo.

Alibainisha kuwa inadaiwa watuhumiwa hao baada ya kuvamia shambani wakiwa na silaha za jadi zikiwamo mapanga, mikuki na mishale waliwajeruhi watu 11 sehemu mbalimbali mwilini mwao ambao wanane kati yao walitibiwa na kuruhusiwa na watatu wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbarali.

Aidha, baada ya kutekeleza uhalifu huo watuhumiwa hao pia walifanya uharibifu wa pikipiki tano ambazo ni mali za wanakijiji cha Mahalala.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Na Joachim Nyambo, Mbeya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi