loader
Picha

SUZA; matokeo ya kutafsiri kwa vitendo Mapinduzi

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ni matokeo ya kutafsiri kwa vitendo, dhamira ya kupanua fursa ya elimu Zanzibar baada ya Mapinduzi ya 1964.

Dk Shein aliyasema hayo jana katika hafla ya kusherehekea mafanikio ya SUZA iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Dk Ali Mohamed Shein uliopo katika Kampasi ya chuo kikuu hicho, Tunguu, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Katika maelezo yake, alisema Chama cha Afro Shirazi Party (ASP), kilikuwa na dira na malengo ya muda mrefu ya kuandaa rasilimali watu ya kuitumikia nchi hii na kusukuma mbele maendeleo yake.

Aliongeza kuwa malengo hayo ya kizalendo yaliyotangazwa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Mzee Abeid Amani Karume, Januari 23, 1964 yameweza kufanikiwa hatua kwa hatua kutokana na dhamira ya dhati ya viongozi waliopo ambao kwa pamoja wamechukua hatua madhubuti za kuimarisha maendekeo ya elimu nchini.

Alieleza kuwa hali hiyo imechochea kuwepo kwa hatua za kuimarisha sekta ya elimu kwa kuzifungua fursa za kuanzisha vyuo vikuu hapa Zanzibar kwani kabla ya mwaka 1998, Zanzibar haikuwa na chuo kikuu hata kimoja na vijana wachache waliobahatika walilazimika kuifuata fursa ya kusoma vyuo vikuu nje ya Zanzbar.

Alisema uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Tano wa Dk Salmin Amour Juma ulifanya uamuzi wa kuanzishwa kwa vyuo vikuu nchini kwa kuruhusu kuanzishwa kwa vyuo vikuu viwili vya binafsi mwaka 1998.

Rais Shein alisema kwa lengo la kutimiza matakwa ya kisheria na mamlaka aliyonayo, Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Sita, Dk Amani Abeid Karume alizindua rasmi Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar mwaka 2001 na kumpongeza kwa mchango wake mkubwa alioutoa kiongozi huyo akiwa mkuu wa kwanza wa chuo hicho.

Dk Shein ambaye pia ni Mkuu wa chuo hicho alieleza kuwa ni dhahiri mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 18 ni ya kupigiwa mfano na ni makubwa ambayo yakwenda sambamba na malengo yaliyowekwa na serikali wakati kilipoanzishwa chuo hicho.

Aidha, alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Saba ilipoingia madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 iliendeleza jitihada za kuimarisha elimu ya juu pamoja na kukiimarisha chuo hicho kwa kuzingatia mipango ya maendeleo ya Zanzibar ikiwemo Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2010-2015.

Rais Shein alitoa pongezi kwa Baraza la Mapinduzi kwa kutoa mwongozo wa kisera wa kukiimarisha chuo hicho

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Maalumu, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi