loader
Picha

Walimu wahamasishwa kutumia benki yao

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameitaka Benki ya Biashara ya Walimu (MCB) kutoa huduma zinazojibu changamoto wanazokumbana nazo walimu katika huduma za kibenki hasa mikopo.

Akizungumza katika kongamano la kuhamasisha walimu kujiunga na huduma za benki hiyo, Profesa Ndalichako alisema mateso na changamoto kubwa walizokumbana nazo walimu kwenye benki hasa wanapochukua mikopo zinapaswa kuwa historia watakapojiunga na Benki ya Biashara ya Walimu.

Alisema walimu wamepata shida kubwa wengine kufilisiwa mali zao kwa kuchukua mikopo ambayo wameshindwa kurejesha kutoka na riba kubwa huku wakichukua mikopo bila kusoma masharti ya mikopo wanayochukua.

Sambamba na hilo, ameitaka benki hiyo kuhakikisha kuwa faida zinazotolewa ikiwemo gawio linalotokana na hisa za wanachama linaonekana wazi ili kuwavutia wateja kujiunga na huduma za benki hiyo.

Akitoa taarifa kwa waziri, Mtendaji Mkuu wa MCB, Richard Makungwa alisema mpango wa benki hiyo ni kuhakikisha walimu wanajiunga na huduma za benki hiyo kwa wingi iwezekanavyo na kufaidi huduma walizonazo.

Makungwa alisema benki imezingatia changamoto mbalimbali za huduma za kibenki zilizokuwa zikiwakabili walimu ikiwamo mikopo yenye masharti magumu na kuwataka walimu waione benki hiyo kama sehemu ya maisha yao.

Mwalimu Mary Nikodem kutoka wilayani Kibondo alihoji mkakati uliowekwa na Benki ya MCB kushawishi na kuvutia walimu kujiunga na huduma za benki hiyo ambayo haina matawi mikoani wala huduma zake hazijulikani huku wateja walionunua hisa wakishindwa kufaidika na gawio.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Na Fadhili Abdallah, Kigoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi