loader
Picha

LATRA waja na muarobaini wa uchezeaji vidhibiti mwendo

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafi ri Ardhini (LATRA) inatarajiwa kuingiza mfumo bora wa udhibiti wa mwendo kwa usafi ri wa mabasi nchini utakaosaidia kudhibiti uchezeaji wa vifaa hivyo unaofanywa na madereva.

Akizungumza katika mkutano wa dharura ulioit ishwa na Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) kujadili kanuni za usafirishaji wa abiria jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Udhibiti Huduma za Barabara wa LATRA, Johansen Kahatano alisema kwa sasa wapo katika hatua za mwisho kabla ya kifaa hicho kuanza kutumika.

Alisema kutokana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika vifaa mbalimbali vya ufuatiliaji wa mwenendo wa mabasi kuchezewa, waliona vyema kuja na kifaa hicho cha kitaifa kwa lengo la kumaliza changamoto hiyo iliyodumu kwa muda mrefu.

Alisema hatua ya ujio wa kifaa hicho umetokana na mapendekezo ya baadhi ya wadau mbalimbali walioona kuna haja ya kuwa na kifaa hicho kupunguza kama siyo kumaliza tatizo la ajali zitokanazo na mwendokasi wa mabasi.

Alisema kifaa hicho kwa sasa kimepelekwa Shirika la Viwango (TBS) kwa ajili ya uchunguzi wa ubora wake kabla hakijaanza kutumika rasmi wakati wowote kuanzia hivi sasa.

Alisema moja ya sifa ya kifaa hicho ni pamoja na kulifanya gari kukata mafuta pale dereva wake atakapokuwa amezidisha mwendo na baadae kuendelea tena ikianza na mwendo wa kawaida.

Aidha, aliwataka wamiliki hao kutumia mfumo unatumika hivi sasa wa VTS kwa ufasaha kutokana na umuhimu wake katika kuhakikisha mwendo wa mabasi unakuwa katika viwango vilivyoelekezwa.

Awali Katibu Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu aliitaka LATRA kufuta baadhi ya vifungu katika kanuni zake ikiwemo ile inayoweza kumfanya mmiliki wa basi kufutiwa leseni kutokana na kosa linaloweza kusababishwa na dereva.

Aidha, pendekezo jingine la TABOA ni pamoja na kumtaka dereva kuendesha basi kwa umbali wa kilometa 700 badala ya ile ya kutoendesha baada ya saa nane inayopendekezwa na sheria ya LATRA.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Na Oscar Job

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi