loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuchukue tahadhari ya ugonjwa wa ebola

JUZI iliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii juu ya watu waliodaiwa kufa kutokana na ugonjwa hatari wa ebola.

Hata hivyo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jana ilitoa taarifa kuuthibitishia umma kuwa hakuna mtu hata mmoja ambaye amekufa kwa ugonjwa huo.

Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri, Dk Faustine Ndugulile wakiambatana na Mganga Mkuu wa Serikali, Mohammed waliueleza umma kuwa ugonjwa huo haujaingia nchini lakini jamii ichukue tahadhari kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwa salama.

Binafsi naamini kwamba sio serikali pekee ambayo inapaswa kutunza usalama wa jamii dhidi ya magonjwa Bali ni jambo la jamii nzima kushiriki.

Ikumbukukwe kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) imetaja DRC nchi miongoni mwa nchi ambazo zilizokumbwa na ebola, na Tanzania inapakana katika baadhi ya mikoa na nchi hiyo.

Nchi hizi mbili zinamuingiliano wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na wa kibiashara na kijamii ambapo ni rahisi kwa mtanzania kuingia DRC na pia kwa raia au mkazi wa DRC kuingia Tanzania.

Tabia ya wananchi kupokea wageni kiholela na kuwahifadhi ni mambo ambayo kama hayatazingatiwa katika kipindi hiki ni hatari kwamba tutaiweka nchi yetu katika hatari ya kuingia ugonjwa huo hatari.

Niwakumbushe watanzania wenzangu kuchukua tahadhari katika suala hili ni muhimu zaidi tukishirikiana na serikali nayo ikafanya yale ambayo yatakua ya upande wake.

Wizara ya Afya imewaomba wananchi mbali na kuchukua tahadhari katika muingiliano huo, pia kutoa taarifa pale ambapo wataona dalili za mgonjwa ambazo zinaendana na zile za ugonjwa wa ebola ambazo ni kuumwa kichwa, homa, kutapika na kutokwa damu katika matundu ya mwili.

Tahadhari iliyotolewa na serikali muhimu kuifuata na kuizingatia.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: Na Regina Mpogolo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi