loader
Picha

Ufundi stadi kwa njia ya uanagenzi wafanyika kwa vijana 5,875

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imetoa mwongozo na maelekezo kwa mabenki na mifuko ya uwezeshaji nchini kuhakikisha inatoa mikopo kwa vikundi vya vijana kwa riba nafuu

Pia amewaagiza wakuu wa mikoa kuandaa orodha ya vijana waliopata mafunzo ya ufundi stadi ili kuwaunganisha na fursa pindi wawekezaji wanapokuja katika mikoa yao.

Majaliwa aliyasema hayo wakati wa kufungua awamu ya pili ya mafunzo ya ufundi stadi kwa njia ya uanagenzi yatakayojumuisha vijana 5,875 yaliyofanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 100 ya Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Alisema ili kuwajengea mazingira mazuri vijana wa kitanzania, wametoa mwongozi na maelekezo kwenye taasisi hizo ili wale wenye mlengo wa kujiajiri kwa kuanzisha taasisi zao wapate mitaji.

“Mkimaliza mafunzo yenu mnauhakika wa kuajiriwa na kujiajiri, mnaweza kujiunga kwenye vikundi vya watu watano hadi kumi mkiwa na maandiko yenu.

Tumeshatoa mwongozo na maelekezo wa benki zetu zote na mifuko ya uwezeshaji kupokea maandiko mradi yenu wayapitishe ni kutoa ushauri na pia watoe mikopo kwa riba isiyo kubwa. T

unataka wote muingie katika sekta ya ajira kwa kujiajiriwa na kujiajiri,” alisema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa kuwa na orodha ya vijana waliopata mafunzo ya uanagenzi na kuwa orodha hiyo itasaidia vijana kupata ajira pindi wawekezaji wanapofika kwenye mikoa husika badala ya kuja na wafanyakazi kutoka maeneo mengine.

“Mkimaliza mafunzo yenu mwende moja kwa moja kwa makatibu tawala wa wilaya ili waawaingize kwenye orodha ya vijana wenye fani ya ufundi stadi na yeye apeleke kwa RAS (Katibu tawala ) mkoa ili mkoa ujue idadi ya vijana walionao, pindi makongamno yanapotokea ya wawezeji wawaelekeze wawekezaji vijana walionao na sifa zao, ilifursa zinapotolewa wawekezaji wasichukuliwe na watu wengine bali wachukuliwe hawa,” alisema.

Alisema serikali imetoa fursa ya ajira kwa wazawa kwa asilimia kubwa na kwamba wafan yakazi wa nje watakaofanya kazi nchini ni wale wenye ujuzi ambao haupatikani nchini.

Alisema takwimu za sasa zinaonesha kuwa chini ya asimilia 10 ya vijana wa Tanzania hawana ajira na kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wanapunguza changamoto hiyo kwa kuwapa ujuzi vijana na kutekeleza mikakati kadhaa.

Alisema Sera ya Taifa iliyozaliwa upya mwaka 2008 imelenga kuhakikisha Watanzania wananufaika na fursa za ajira zinazopatikana ndani na nje ya nchi kwa kuwawezesha wananchi hususan vijana kupata ujuzi; mikopo kupitia mifuko mbalimbali na kupata maeneo ya kufanyia shuguli za kiuchumi.

Akizungumzia mafunzo hayo, Majaliwa alisema zaidi ya vijana 46,000 wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya stadi za kazi kwa njia ya uanagenzi kupitia Taasisi ya Don Bosco Net Tanzania katika mwaka huu wa fedha.

Alisema miongoni mwa mafunzo yanayotolewa chini ya programu hiyo ni ya uanagenzi (apprenticeship) ambayo yalianza 2017 na 2018 walihitimu vijana 32,786 huku awamu ya pili ya mafunzo hayo yaliyozinduliwa jana yanahusisha jumla ya vijana 5,875 kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 ya ILO.

Alisema miongoni mwa sababu zinazotajwa kuchangia ukosefu wa ajira kwa vijana ni vijana kutokuwa na ujuzi sahihi wa kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema hadi kufikia Juni 2019, vijana 36,726 wamefaidika na programu ya kukuza ujuzi inayogharamiwa na serikali kwa asilimia 100.

Alisema kati yao vijana 6,455 walinufaika na mafunzo ya uanagenzi katika fani mbalimbali zikiwemo za ushonaji na nguo, useremara, uashi, terazo, uchongaji wa vipuri, ufundi magari, umeme na utengenezaji wa viatu vya ngozi.

Naye Mratibu wa Miradi wa Taasisi ya Donbosco Tanzania, Rosemary Njoki alisema programu ya kukuza ujuzi imezingatia kuwawezesha vijana wa miaka kati 17 hadi 35 kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa.

Mkurugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki, Wellington Chibebe alisema shirika hilo limedhamiria kupigania haki ya kijamii pamoja na haki za binadamu na kazi zinazotambulika kimataifa.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Na Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi