loader
Picha

Vijana wachagizwa kuwania uongozi uchaguzi serikali za mitaa

VIJANA wilayani Muheza mkoani Tanga wametakiwa kuchangamkia fursa za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika vyama vya siasa katika chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Salome Zuakuu amebainisha kuwa vijana wanayo nafasi kubwa katika nafasi za uongozi.

Aliyasema hayo wakati akizungumzia maandalizi ya sherehe ya uzinduzi wa Kampeni ya “Muheza ya Kijani” yenye kaulimbiu “Vijana Tukithubutu Tutaweza.”

Alibainisha kuwa vijana wenye sifa za kuombea uongozi wanatakiwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za Serikali za Mitaa kwani ndio fursa pekee ya kuanza kuamka kiuongozi kwao.

Katika uzinduzi wa kampeni hiyo takribani vijana 1,000 kutoka katika kata zote 37 za Wilaya ya Muheza wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo.

Aliongeza maangalizi yote ya sherehe hizo yamekamilika na mambo mengi yatakayozungumzwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020 katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya nchi.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Na Cheji Bakari, Tanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi