loader
Picha

Yanga yajiweka mtegoni

MCHEZAJI wa zamani wa Yanga, Thabani Kamusoko jana aliinyima ushindi timu yake hiyo baada ya kuifungia Zesco ya Zambia bao la kusawazisha katika dakika za majeruhi za mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga ilikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa kwa penalti katika dakika ya 25 na Patricl Sibomana baada ya mchezaji mwigine wa timu hiyo, Sadney Urikhob kuangushwa katika eneo la hatari.

Kamusoko, ambaye alijiunga na Yanga mwaka 2016 kabla ya kuondoka baada ya misimu kadhaa, alifunga bao hilo la kusawazisha katika dakika ya 90 na kuiwezesha timu yake kumaliza kwa sare ya 1-1.

Kwa matokeo hayo, Yanga sasa ina kibarua kigumu kuhakikisha inatoka sare ya kuanzia mabao 2-2 au kushinda kwa idadi yoyote ya mabao katika mchezo wa marudiano ugenini, ili kusonga mbele katika hatua ya makundi.

Hatahivyo, endapo Yanga itatolewa na Zesco katika Ligi ya Mabingwa, itaangukia katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kama ilivyofanya msimu miwili iliyopita.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alikiri timu yake kupoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga, lakini alisisitiza hilo haliwafanyi timu ya kushindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Zambia.

Alisema atahakikisha timu yake hairudii makosa ya kukosa mabao kibao mbele ya lango la wapinzani wake.

Naye kocha wa Zesco, Godfrey Lwandamina aliionya Yanga na kusema kuwa timu yake haijawahi kupoteza mchezo wowote wa kimataifa kwenye Uwanja wa Mwanawasa nchini Zambia, hivyo wapinzani wao waende Zambia kwa tahadhari kubwa.

Lwandamina aliwahi kuiifundisha Yanga na kuondoka miaka miwili iliyopita na kurudi kwao Zambia.

Yanga ilipoteza nafasi katika dakika ya nne na 15 wakati Sadney Urikhob aliposhindwa kufunga licha ya kuwa katika nafasi nzuri.

Dakika ya nne Mapinduzi Balama alikosa bao katika dakika ya 11 huku Papy Tshishimbi naye akishindwa kuujaza mpira wavuni katika dakika ya 56.

Kikosi Yanga: Metacha Mnata, Ally Mtoni, Kelvin Yondani, Feisali Salum, Mapinduzi Balama/Ally Ally, Mohamed Issa/Ngassa, Patrick Sibomana, Sadney Urikhob/Maybin Kalengo, GWIJI

foto
Mwandishi: Na Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi