loader
Picha

Azam washtukia mtego Caf

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrka, Azam FC imesema itahakikisha inautumia vema uwanja wake wa nyumbani kwa kupata mabao mengi kadiri wawezavyo ili yawasaidie kuwavusha katika hatua inayofuata.

Azam FC leo Jumapili itawaalika Triangle United FC kwenye dimba la Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni kucheza mechi ya kwanza ya hatua ya kwanza kusaka nafasi ya kutinga hatua ya mtoano.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Mtendaji Mkuu wa Azam , Abdulkarim Nurdin ‘Popat’ alisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakishindwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani kwa kupata ushindi wa mabao machache na wakienda ugenini wanafungwa mabao mengi na kutolewa.

Aliweka wazi kuwa msimu huu wanataka kukwepa mtego huo na wameona njia pekee ni kupata mabao mengi nyumbani ili mechi za ugenini zisiwe ngumu kwao.

Aliongeza kuwa kikosi cha Azam kwasasa kimeongezeka makali baada ya wachezaji wao Mudathir Yahya pamoja na David Mwantika kuanza mazoezi baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakiwasumbua.

“Tulishinda 2-0 hapa nyumbani dhidi ya Al Mareikh lakini tulipokwenda kwao tukafungwa 3-0 na kutolewa, pia Esparence walitutoa baada ya kuwafunga hapa nyumbani 2-1, kwao wakatufunga tatu, tumeona mabao machache hayatoshi hivyo angalau tupate matokeo ya kuanzia 3-0 na kuendelea,” alisema Popat.

foto
Mwandishi: Na Mohammed Mdose

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi