loader
Picha

Maswali kibao Kujiuzulu Nkwabi Simba

MASWALI kibao yameibuka baada ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Swedi Mkwabi (pichani) kujiuzulu katika nafasi hiyo jana kwa kile alichoeleza kuwa anataka kufanya majukumu yake binafsi ikiwa ni mwaka mmoja tangu alipoanza kuitumikia klabu hiyo.

Taarifa iliyotolewa jana na Simba ilisema kuwa Mkwambi aliuandikia barua uongozi wa Simba akieleza kufanya maamuzi hayo kwa hiari yake na kwamba hatua hiyo imekuja kwa kile alichodai kuhitaji muda zaidi wa kusimamia shughuli zake.

Uongozi wa klabu hiyo kupitia bodi ya wakurugenzi na sekretarieti umebariki uamuzi wake na kumtakiwa kila la kheri na kwamba wanaimani atakuwa mshiriki mzuri wa masuala mbalimbali ya klabu hiyo.

Simba ilisema utaratibu wa kumpata mwenyekiti mwingine utatangazwa hapo baadaye ili kujaza nafasi hiyo ya Mkwambi aliyekuwa madarakani kwa msimu mmoja pekee.

Mkwabi anakuwa kiongozi wa pili kuondoka katika klabu hiyo baada ya mtendaji mkuu, Crescentius Magori kuondoka wiki moja iliyopita baada ya mkataba wake kumalizika na nafasi yake kuchukuliwa na Senzo Mazingiza kutoka Afrika Kusini.

Alitangazwa kuwa mwe- nyekiti wa klabu hiyo November 5, mwaka jana baada ya kushinda nafasi hiyo kwa asilimia 51% ya kura zilizopigwa na wanachama 1728, katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es salaam.

Katika kampeni yake ya kwanza iliyofanyika mwaka jana Hotel ya Southern Sun, Mkwabi aliahidi kutafuta njia mbalimbali za mapato ya klabu hiyo ikiwemo, uanzishaji na uuzaji wa mabegi, jezi na vifaa vingine vya michezo.

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

1 Comments

  • avatar
    apolinali kamwanga
    17/09/2019

    viongozi wengine wanataka kazi kwaajiri ya maslahi binafsi,wengine ni kwamaslahi ya tem,ukitokea utofauti,utaona wengine wanajihuzuru,(KUNA JIPU HAPO)wana simba kaeni vizuri hapo.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi