loader
Picha

SGR kukomboa wafugaji

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na ufufuaji wa reli ya zamani ni mkombozi kwa wafugaji na wafanyabiashara ya mifugo nchini, hasa katika kufi kia masoko na kupunguza gharama za usafi rishaji.

Alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipotembelea ujenzi wa reli ya SGR pamoja na eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya bandari kavu, eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kushushia na kupakia mifugo kutoka shamba la kupumzishia mifugo la serikali lililopo Kata ya Kwala, Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani.

Naibu Waziri Ulega alisema ujenzi huo umefika wakati muafaka kwa kuzingatia kwamba kadri sekta ya mifugo inavyozidi kukua inahitaji huduma za usafirishaji kwa gharama nafuu kumwezesha mlaji kuwa na bei inayowezekana.

“Reli ya zamani ilikuwa na miundombinu yote inayohusisha mifugo na reli yetu ya kisasa SGR iendelee kuhusisha mifugo na ufufuaji wa reli ya zamani uende sambamba na kujua kwamba mifugo yetu ndio malighafi kwa viwanda vya usindikaji nyama,”alisema.

Katika ziara hiyo ambayo pia Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye alikuwepo; Ulega alisema ujenzi wa reli hiyo ya kisasa mara utakapokamilika na kuanza kufanya kazi, pato la taifa litakua kupitia sekta ya mifugo kwa kuwa mifugo itakuwa inasafirishwa kwa haraka.

Kwa upande wake, Nditiye alisema wizara yake imepata mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 300 kwa ajili ya kufufua reli ya zamani, hivyo itahakikisha wakulima na wafugaji wanatumia ipasavyo SGR pamoja na reli ya zamani.

Nditiye alimuomba Naibu Waziri Ulega kufikisha wataalamu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika eneo la bandari kavu lililopo Kata ya Kwala wilayani Bagamoyo, ambalo limetengwa maalumu kwa ajili ya mifugo ili wataalamu hao watoe muongozo wa michoro ya namna eneo hilo linavyopaswa kuwa.

Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania, Maghembe Makoye aliishukuru serikali kwa ujenzi wa reli ya kisasa kwa kuwa mifugo itakuwa inasafirishwa kwa muda mfupi na kufika katika eneo husika ikiwa na afya njema.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Bagamoyo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi