loader
Picha

TIC- Dar imejaa, Pwani itumike uwekezaji mkubwa

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kimesema, mkoa wa Pwani una fursa nzuri ya kutumika kwa uwekezaji mkubwa kwa sababu bado una nafasi kulinganisha na Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Geoffrey Mwambe amesema jijini Dar es Salaam kuwa, mkoa huo pia una sifa kubwa ya utayari wake wa kupokea uwekezaji kwenye maandalizi ya ardhi.

“Pwani haina mkoa mwingine wa kushindana nao, hata Dar es Salaam yenyewe haiwezi ku-compete (kushindana) na Pwani kwa sababu Dar es Salaam haina hilo eneo na haitoi hiyo fursa ya viwanda kuwepo”amesema Mwambe kwenye ofisi za TIC jijini Dar es Salaam.

Amesema, ukaribu wa Pwani na Dar es Salaam pia ni faida kubwa kwa Pwani kwa ajili ya wawekezaji wanaotaka Dar es Salaam iwe soko lao, uwepo wa bandari kwa ajili ya kuuza bidhaa nje au kuleta malighafi.

“Na hii ni kwa sababu Dar es Salaam imejaa na Dar es Salaam zaidi sana ni sehemu ya makazi na soft infrastructure, na viwanda vikubwa vikubwa visogee sehemu ambako kuna nafasi kubwa na pia itasaidia kwa ajili ya emission ya gesi zile, hewa na nini, na pia kupangwe, Dar es Salaam maeneo ya viwanda ilikuwa ni Vingunguti, eti Mikocheni industria area, hayo sio maeneo ya viwanda. Na ukitaka heavy industries sio Dar es Salaam”amesema.

Amesema, TIC inafurahi kuona mikoa inanadi fursa za uwekezaji nchini. Mwambe amesema, jukumu la kuzinadi fursa hizo ni lao (TIC) lakini ni vigumu kufanya kwa wakati kwenye mikoa yote.

“Kimsingi jukumu la kupromote investment opportunities (kunadi fursa za uwekezaji) kwenye nchi hii ni la TIC . Lakini kisheria imetuambia kwamba pia tu-coordinate (turatibu) masuala yote ya uwekezaji kwenye nchi hii”amesema.

Amesema, taasisi mbalimbali zinaweza kufanya kazi ya kunadi fursa za uwekezaji lakini lazima TIC iratibu kazi hizo.

ILI kukabiliana na ugonjwa wa Covid- 19 unaosababishwa na virusi ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi