loader
Picha

Tanzania, Zanzibar kundi moja Cecafa U20

TIMU ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), imepangwa Kundi B katika mashindano ya Afrika Mashariki ya Cecafa 2019 yatakayofanyia Uganda, imeelezwa.

Ngorongoro Heroes katika Kundi B imepangwa na Kenya na Zanzibar katika mashindano hayo yatakayofanyika Uganda kuanzia Septemba 21.

Wakati katika Kundi A kutakuwa na wenyeji Uganda, Sudan, Eritrea na Djibouti huku Kundi C likiwa na timu za mataifa ya Burundi, Sudan Kusini na Somalia.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, timu tatu za juu kutoka katika Kundi A na B zitasonga mbele katika robo fainali na kuungana na timu mbili za kwanza kutoka Kundi C.

Kikosi cha awali cha Tanzania chini ya Kocha Mkuu, Zuberi Katwila chenye wachezaji 35 kinaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo ya Uganda.

Kikosi cha awali cha Ngorongoro Heroes: Ramadhan Kabwili – Yanga, Ally Salim – Simba, Abdul Seleman-U18, Oscar Masai – Azam, Lusajo Mwaikenda – Azam, Dickson Job – Mtibwa, Gustapha Simon – Yanga, Onesmo Mayaya – Mtibwa, Kelvin Kijiri – KMC na James Kahimba – Coastal Union.

Wengine ni Ally Msengi – KMC, Ally Ng’anzi – Madison (Marekani), Kelvin Nashon –JKT, Lenny Kissu – Biashara, Yahya Mbegu – Simba, Frank Kahole – Mtibwa, Andrew Simchiba – Coastal, Mohamed Abdllah – Mtibwa, Razack Ramadhan –Mtibwa, Wilbore Maseke – Azam na Gadafi Said – Azam.

Wengine ni Novatus Dismas – Biashara, Abubakar Juma – Mtibwa, Israel Mwenda – Alliance, Samwel Jackson – Azam, Omar Banda – Azam, Kassim Shaban – Sahare, Kibwana Shomari – Mtibwa, Tariq Seif – Biashara, Agiri Ngoda – Azam, Tepsi Evance – Azam, Nickson Kibabage – Al Jadida, Morocco Zanda Said – Azam, Kelvin John -U17 na Herbert Lukindo-Mbao.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi