loader
Picha

Askofu Mkuu Ruwai’chi atolewa ICU

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Thadeus Ruwai’chi ametolewa chumba cha uangalizi maalumu (ICU) na kupelekwa wodi za kawaida.

Jopo la wataalamu 7 waliokuwa wanamhudumia Askofu Mkuu Ruwai’chi limeamua hivyo leo asubuhi baada ya kujiridhisha kuwa hali ya kiongozi huyo inaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano cha Taasisi ya Mifupa (MOI) kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) madaktari wameamua hivyo baada ya kufanyika tathimini ya vipimo na maendeleo yake.

“Taasisi ya MOI inawahakikishia Watanzania hususani waumini wa kanisa Katoliki kuwa Askofu Ruwai’chi yuko salama na hali yake imeimarika sana hivyo waendelee kumuombea ili arejee kwenye majukumu yake,” imeeleza taarifa hiyo.

Jopo linalomhudumia Askofu Ruwai’chi ni pamoja na madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo, madaktari bingwa wa usingizi, madaktari bingwa magonjwa ya ndani, wataalamu wa lishe, wauguzi wabobezi na wataalamu wa mazoezi tiba.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi