loader
Picha

Kikosi cha maangamizi Taifa Stars hadharani

KOCHA Mkuu wa timu ya Soka ya Taifa, Taifa Stars, Etienne Ndayi- ragije, ametangaza kikosi cha wachezaji 20 watakaoingia kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Sudan inayaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.

Katika kikosi hicho, kocha huyo wa muda amemwita Mzamiru Yas- sin wa Simba, ikiwa ni muda mrefu umepita tangu kuachwa kwenye kikosi cha Stars. Mechi hiyo ni ya kuwania fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani Chan, 2020.

Wachezaji wengine walioitwa kikosini ni Juma Kaseja (KMC), Metacha Mnata (Yanga ), Saidi Kipao (Kagera Sugar), Haruna Shamte, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Miraji Athumani, Mzamiru Yassin na Gadiel Michael (Simba). Kelvin Yondani, Mohammed Issa, Abdul Makame na Feisal Salum (Yanga), Iddi Seleman, Mudathir Yahya, Salum Abubakar, Frank Domayo na Shaaban Chilunda (Azam).

Wengien ni Ayoub Lyanga, Ba- kari Nondo kutoka Coastal Union, Iddi Mobi na Baraka Majogoro kutoka Polisi Tanzania na Boniface Maganga wa KMC.

Kikosi hicho kilitarajiwa kuingia kambini jana. Mshindi wa mechi hiyo itakayochezwa nyumbani na ugenini atafuzu hatua ya makundi.

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

1 Comments

  • avatar
    apolinali kamwanga
    17/09/2019

    kikosi nimekipenda,kocha kamsahau mmoja,(IDD KIPAGWILE)

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi