loader
Picha

Cecafa yazihakikishia usalama timu za U20

KATIBU Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Nicholas Musonye, amewahakikishia usalama wao washiriki wote wa mashindano yajayo ya Kombe la Chalenji kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20.

Kenya ni miongoni mwa timu 11 kutoka nchi wanachama zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo yatakayoanza kutimua vum- bi katika viwanja mbalimbali kuanzia Septemba 21 nchini Uganda.

Mashindano hayo yata- pigwa kwenye miji tofauti tofauti kama Jinja jirani na Mto Nile, na Gulu, Kaskazini ya Uganda ikiwa ni kilometa 350 kutoka mji mkuu wa Kampala.

Kaskazini ya Uganda huwa kuna matatizo ya kiusalama na wiki iliyopita, Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Uganda, Yow- eri Museveni, walishuhudia utiaji saini wa kuendeleza amani kuelekea maende- leo kati ya mikoa iliyopo mpakani.

“Kuna amani kubwa huko Gulu, huo ndio ukweli. Tunajua tunachokifanya. Haya mashindano tumeya- panga pamoja na wenzetu katika ukanda huu. Tunawa- toa shaka watu kadhaa Gulu na Jinja ambao wanataka kuangalia mashindano haya, subirini na mtaona umati wa watu,” alisema.

Na kuhusiana na hilo, mshambuliaji wa Kenya Musa Masika anasema timu yake haimuhofii yeyote. Kundi A: Uganda, Sudan, Eritrea na Djibouti Kundi B: Kenya, Ethiopia, Zanzibar na Tanzania Kundi C: Burundi, Sudan Kusini na Somalia.

UONGOZI wa klabu ya Chelsea umempa ruhusa kiungo wake N’golo ...

foto
Mwandishi: KAMPALA, Uganda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi