loader
Picha

Mukura yaiduwaza Rayon kwa kichapo

MUKURA Victory Sports ndio washindi wa taji la mwaka huu la mashindano ya Aga- ciro baada ya kuifunga Rayon Sports 2-1 katika fainali iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Amahoro.

Kipigo hicho cha kushtua kwa Rayon Sports ni cha pili kutoka kwa Mu- kura katika fainali, mara ya kwanza timu hizo zikikuta- na katika fainali za Kombe la Amani mwaka 2018 na mchezo huo kuamriwa kwa penati kwenye Uwanja wa Kigali.

Kipigo hicho kinaizuia Rayon Sports kwa mara ya tatu mfululizo kutwaa taji hilo la Agaciro. Baada ya kuanza kip- indi cha kwanza taratibu, mshambuliaji, Samuel Chukwudi, alifunga bao la kuongoza katika dakika ya 49 na kuifanya Mukura kuwa mbele kabla, Inno- cent Ndizeye, hajaongeza ushindi huo kwa mkwaju wa penati baada ya dakika tatu.

Mwamuzi wa kati, Sam- uel Uwikunda, hakusita ku- toa penati baada ya beki wa zamani wa Mukura, Saidi Iragire, kuunawa mpira ndani ya boksi.

Dakika 10 baadae, Mi- chael Sarpong, alifunga bao la kufutia machozi katika mashindano ya mwaka 2017 na lile la ushndi la mwaka jana, naye alifunga kwa njia ya penalti baada ya Alex Ngirimana kuuzuia kwa mkono mpira wa krosi kutoka kwa Hussein Habimana.

“Nimefurahi sana kush- inda taji hili kwa mara ya kwanza nikiwa na Mukura, hili ni jambo zuri sana wakati tukijiandaa kwa msimu mpya wa Ligi Kuu,” alisema kocha Mcameroon Olivier Ovambe baada ya mchezo huo.

Timu zote zilimaliza mchezo huo zikiwa pun- gufu, wakati Rayon Sports ikimpoteza nahodha wao, Eric Rutanga, baada ya kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika dakika ya 70 baada ya kum- tukana mwamuzi wakati mfungaji wa Mukura, Ndizeye alitolewa katika dakika ya 77 baada ya ku- pewa kadi ya pili ya njano.

Wakati huohuo, timu ya polisi ambayo ilitwaa taji hilo wakati mashindano hayo yakichezwa kwa mara ya kwanza mwala 2015, ilimaliza ya tatu baada ya kuifunga APR 1-0, shukrani kwa bao pekee lililofungwa na Osée Iyabivuze katika dakika ya 73.

UONGOZI wa klabu ya Chelsea umempa ruhusa kiungo wake N’golo ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi