loader
Picha

Minziro, Chambua wazikosoa Yanga, Azam

Nyota wa Zamani wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Sekilojo Chambua na Fred Minziro, wamesema pamoja na makocha wa vikosi vya Yanga SC na Azam FC kuwatoa hofu mashabiki na kuwajaza matumaini ya kwenda kupindua matokeo katika mechi za marudiano za kimataifa, wanapaswa kutegua kitendawili kilichowakosesha ushindi kwenye michezo ya awali.

Wiki iliyopita timu hizo zilikosa ushindi katika mechi za nyumbani, ambapo Yanga inayocheza Ligi ya Mabingwa Afrika ilitoka sare ya bao 1-1 na Zesco ya Zambia na Azam inayocheza michuano ya Kombe la Shirikisho ilifungwa bao 1-0 na Triangle ya Zimbabwe.

Matokeo hayo yameziwe- ka timu hizo kwenye wakati mgumu, kwani zitalazimika kushinda katika mechi za marudiano wiki ijayo kama zinataka kusonga mbele.

Baada ya mechi hizo, kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera na yule wa Azam,Etienne Ndayiragije, wamet- amba kupindua matokeo ka- tika mechi za marudiano na kusonga mbele, wakidai kila timu ina uwezo wa kushinda kwao.

Chambua alisema, kwa matokeo waliyoyapata Yanga kwenye mchezo wao wa kwanza, wameifanya mechi ya marudio kuwa ngumu kwao ingawa kwenye mpira lolote linaweza kutokea.

Alisema wasiwasi wake katika mchezo huo unakuja kufuatia kikosi hicho kukosa muendelezo mzuri wa kupata matokeo chanya yanayochangiwa na ubutu wa safu ya ushambuliaji kushindwa kufunga kila wanapopata nafasi.

“Kwa ujumla kikosi cha Yanga kwa asilimia kubwa kinaundwa na wachezaji wa- geni, lakini hata hivyo kocha wao hajafanikiwa kuungani- sha timu hadi sasa. Matokeo wanayoendelea kuyapata sio taswira nzuri kwao.”

“Na pili wachezaji na kocha wanapaswa kujiuliza kwanini hawafungi, kikosi kimekosa mfungaji hivyo wana kazi ya ziada ya ku- fanya kama ilivyokuwa kwa Township Rollers,” alisema Chambua.

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi