loader
Picha

Miamba Ulaya yaanza mbio Ligi ya Mabingwa

HATUA ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inaanza leo na mabing- wa watetezi Liverpool wakisaka nafasi ya kute- tea taji lao watakapoanza kampeni zao kwa kucheza ugenini dhidi ya Napoli.

Mbali na Liverpool, vigogo vingine vya Ulaya kama Inter Milan, Chelsea, Valencia, Barcelona na Borus- sia Dortmund ni baadhi ya timu zitakazoshuka dimbani leo kuanza kampeni zao za kuwania taji hilo.

Hatua hiyo ya makundi itaendelea tena kesho kwa vigogo Juventus, Atletico Madrid, Bayern Leverkusen, mabingwa wa England na Ujerumani, Man City na Bay- ern Munchen, vitaanza mbio za kusaka nafasi ya kucheza fainali itakayofanyika Istan- bul, Uturuki mwakani.

Mfumo wa timu 32 hatua ya makundi unapelekea kuchezwa kwa hatua ya 16 bora, ambao ulianzishwa huo hakuna timu zilizokuwa katika kundi dogo kuwahi kutwaa taji hilo, huku mataji 15 ya mwisho yalibebwa na klabu kutoka Hispania, Eng- land, Ujerumani na Italia.

Sasa Chama cha Klabu Ulaya ambacho kinaon- gozwa na kiongozi wa klabu ya Juventus, Andrea Agnelli, kimekuwa na kazi nyingi na Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) ikiwamo kufanya mabadiliko makubwa ya mashindano hayo yatakayo- anza 2024.

Katika ratiba ya leo, mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, Liv- erpool wenyewe wataanza kampeni zao kwa kucheza ugenini dhidi ya Napoli ya Italia katika mchezo unao- tarajia kuwa mgumu na wa kusisimua.

Mabingwa wa Hispania Barcelona, wenyewe wataan- zia Ujerumani kwa kucheza dhidi ya timu ngumu ya Borussia Dortmund katika mchezo mwingine wa kusi- simua, huku Chelsea ya Eng- Inter Milan ya Italia itakuwa mwenyeji wa Slavia Prague.

Zawadi za washindi Kwa sasa, washindi wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya watachukua jumla ya kitita cha Dola za Marekani milioni 83 (ambazo ni sawa na Sh bilioni 190) na mbali na hapo pia wataongezwa fedha zinazotokana na haki ya matangazo ya televisheni kulingana na viwango vya Uefa.

Zawadi hizo ina maana kuwa, inaihakikishia Real Madrid inayoongoza kwa viwango vya ubora kupata fedha zaidi ya Euro milioni 35.46. Kwa bingwa mtetezi Liverpool itapata kiasi cha ziada cha karibu Euro mil- ioni 27.

Uwezo wa kifedha wa timu za juu za Ligi Kuu ya England, ina maana kuwa, timu hizo hazina njaa ya mabadiliko ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na kudhihirisha kwanini timu nne zilizocheza fainali mbili za Ulaya zilikuwa kutoka Uingereza.

Baada ya kuifunga Tot- tenham Hotspur 2-0 huko Madrid na kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya sita, Liverpool inaweza kucheza kwa mara ya tatu mfulu- lizo fainali hizo?, wakati utaamua.

Msimu huu fainali hizo zitapigwa Istanbul. “Tuna nafasi sawa na wengine, lakini huo ndio ukweli timu za Uingereza zinatawala. Nafikiri timu nyingi zina nafasi ya kufanya vizuri,” alisema kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp.

Mashindano haya ni magumu na wachezaji nyota kama Lionel Messi na Cris- tiano Ronaldo hawajawahi kuongoza kwa ufungaji ka- tika katika kipindi cha miaka 12 iliyopita ya mashindano hayo.

Messi sasa ana umri wa miaka 32, amefunga mabao 110 na kushinda taji hilo mara tatu, wakati Ronaldo, hivi karibuni atafikisha miaka 35, ana mabao 123 katika kipindi hicho na ana medali tano za ushindi.

UONGOZI wa klabu ya Chelsea umempa ruhusa kiungo wake N’golo ...

foto
Mwandishi: PARIS, Ufaransa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi