loader
Picha

Mwakyembe apongeza Wamasai kulinda mila

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewapongeza wazee na viongozi wa kimila wa kabila la kimasai kwa kuendeleza na kuhifadhi mila na desturi.

Alitoa pongezi hiyo juzi jijini Arusha wakati wa ku- funga mafunzo ya kimila kwa vijana wa Kimasai. Alisema mafunzo hayo ni muhimu katika kumjenga kijana kuwa mtu mwenye maadili na kuheshimika kwa jamii yake.

“Mafunzo mliyoyapata kutoka kwa viongozi wenu na wazee wa kimila yanawajenga kuwa rai wema na wenye maadili katika kujenga taifa letu, ” alisema Dk Mwakyembe alipowahutubia.

Alisema wizara inaunga mkono juhudi za wazee wa kimasai kwa kuhakikisha mila na desturi ya Mtanzania inatunzwa na kuendelezwa kwa vizazi vijavyo.

Waziri huyo aliahidi kush- irikiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi katika kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za mila yanahifad- hiwa vizuri bila kuingiliwa na watu.

Vilevile aliwapongeza viongozi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuruhusu mae- neo ya kijeshi ambayo ni ya kihistoria kuendelea kutumika kwa ajili ya masuala ya kimila na kuzitaka taasisi nyingine ambazo zina maeneo hayo kuiga mfano huo.

Mwenyekiti wa viongozi wa ukoo wa Wamasai, Isack Lekisongo aliiomba serikali kulinda, kuhifadhi na kuendeleza mila na desturi za jamii mbalimbali za kitanzania ili kupunguza madhara yanayoletwa na utandawazi nchini.

Alisema kupitia mafunzo hayo yanayotolewa kwa vijana yanasaidia kujitambua, kuheshimu wakubwa na wadogo na kuachana na tabia zisizofaa ikiwemo utumiaji wa dawa za kulevya.

Shughuli za kimila za kimasai zilifunguliwa Julai 6, mwaka huu kwa vijana kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na nchi jirani ya Kenya ambao walipewa mafunzo kwa siku 100 yaliyohitimishwa Sep- temba 15, mwaka huu.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi