loader
Picha

‘Ruvuma ina ziada ya chakula’

MKOA wa Ruvuma una ziada ya chakula tani 269,000 kilichozalishwa katika msimu wa kilimo mwaka huu katika magh- ala yake, huku pato la mwananchi katika mkoa huo likipanda kutoka Sh milioni 2.1 mwaka 2015 hadi kufikia Sh milioni 2.24 mwaka huu, kwa mwaka.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme (pichani) alitoakaulihiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea kituo cha ununuzi wa mahindi cha Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea kilichopo eneo la Ruhuwiko mjini Songea.

Alisema mafanikio hayo yametokana na juhudi kubwa za uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara zinazofanywa na wakulima wa mkoa huo ambao wamekuwa wanatumia fursa za kuwepo kwa ardhi nzuri na mvua zinazonyesha kwa wingi kuzalisha mazao mashambani.

Aidha, alitangaza rasmi bei mpya ya mahindi kutoka Sh 430 hadi Sh 600 kwa kilo na kuwataka wakulima kupeleka mahindi yao kwa NFRA ili kupata bei nzuri, badala ya kuuza kwa wafanyabiashara wengine ambao wananunua kwa bei isiyolingana na gharama halisi ya uzalishaji.

Alieleza kuwa serikali imeongeza mgao wa mahindi kwa NFRA kutoka tani 13,000 mwaka jana hadi kufikia tani 25,000 katika msimu wa mwaka huu, uamuzi huo unatokana na kutambua na kuthamini kazi zinazofanywa na wakulima wa mkoa huo.

Katika hatua nyingine, Mndeme alisema serikali imeanza kujenga vihenge na maghala mapya ambayo yatatumika kuhifadhi na kuongeza thamani ya mazao.

Pia, alisema jumla ya watu 600 wamepata vibarua vya muda na kudumu katika kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula wanaofanya kazi mbalimbali, hivyo NFRA imesaidia kupunguza tatizo la ajira kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa NFRA kanda ya Songea, Eva Michael alisema hadi sasa wakala huyo umenunua tani 12,000 za mahindi na wanaendelea ku- pokea mahindi kutoka sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Ruvuma.

Alisema ununuzi wa mahindi unafanyika kwa ubora wa hali ya juu ili kupata mahindi safi ambayo yatakidhi vigezo na kuwataka wakulima kupeleka mahindi kwa wingi kwa NFRA.

Baadhi ya wakulima walio- kutwa wakiuza mahindi yao katika kituo hicho, waliishukuru serikali kwa uamuzi wa kuongeza bei ya mahindi.

Hata hivyo wameiomba kudhibiti uuzaji holela wa pembejeo hasa mbolea ambazo zinauzwa kwa bei kubwa. Rose Mbonde alisema wakulima wamekuwa wakitekeleza maagizo yanayotolewa na serikali yao, hata hivyo wengine wanashindwa kulima kutokana na changamoto ya kupanda kwa gharama za pembejeo jambo linalowakatisha tamaa baadhi ya wakulima.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Songea

1 Comments

  • avatar
    Katturu Adam
    16/03/2020

    Sehemu inayolima mahind kwa wing ruvuma?

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi