loader
Picha

Walimu waliorundikana mjini Ifakara kupelekwa Mlimba

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wiki mbili kwa ofisa elimu wa mkoa wa Morogoro, kuwapanga upya walimu waliopo katika shule za mjini Ifakara ili wengine kwenda shule zilizopo tarafa ya Mlimba wilayani Kilombero.

Hatua hiyo imekuja baada ya kubainika kuwa katika shule za wilayani Mlimba, kuna upungufu wa walimu, hivyo hatua hiyo itaweka uwiano wa ikama kati ya shule za mjini na za vijijini.

Majaliwa alitoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa mji wa Mlimba,waliojitokeza kwa wingi kumpokea, kumsikiliza na kuwasilisha kero zao mbalimbali ikiwemo ya uhaba wa walimu wa shule za msingi.

Akiwa katika tarafa ya Mlimba, Waziri Mkuu alipokea taarifa kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo, Susan Kiwanga (Chadema) pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu CCM , Dk Getrude Rwakatale zinazohusu changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo, ikiwemo maji, barabara na elimu hasa ya uhaba wa walimu wa shule za Msingi.

“Katika kutatua kero ya upungufu wa walimu kwenye shule za tarafa hii namwagiza Ofisa Elimu wa mkoa kuhakiki- sha anawaleta walimu wa kutosha katika Jimbo la Mlimba” alisema Waziri Mkuu.

Katika mkutano huo ,baadhi ya wananchi walio- wasilisha malalamiko yao kwa njia ya maandishi, waliomba serikali kusaidia kupatikana kwa matangazo ya TBC Taifa na TBC FM ili waweze kufua- tilia masuala mbalimbali ya maendeleo .

Waziri Mkuu baada ya kupokea makalamiko hayo, aliwaahidi wananchi wa eneo hilo kuwa suala hilo limefikishwa mahali pake na kwamba atalishughulikia tatizo hilo.

Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu aliagiza wasaidizi wake kutowazuia wananchi wenye kero zao za kufikisha kwa njia ya ujumbe wa mabango, ambapo aliya- soma na kuyatolea majibu.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Kilombero

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi