loader
Picha

Buganda kufanya utafiti wa magonjwa mikoa 6

HOSPITALI ya Rufaa Bugando jijini Mwanza imezindua utafiti maalumu kwa ajili ya magonjwa yasiyoambukizwa, ambapo utafiti huo utafanyika katika wilaya 12 za mikoa sita ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano malumu, Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Profesa Abel Makubi alisema magonjwa hayo yamekuwa ni tatizo kubwa, hivyo wameamua kufanya utafiti ili kuyapatia ufumbuzi. Alisema tafiti hizo zitafanywa na madakari bingwa 12 na wata- fiti wasaidizi 200.

Makubi alisema tafiti hizo zitafanyika katika mikoa sita ya Simiyu, Mwanza, Kagera, Geita, Shinyanga na Mara. Alisema magonjwa yasiyoambukiza ni shinikizo la damu, uzito uliopitiza, magonjwa ya moyo, magonjwa ya figo, kisukari na saratani.

Alitaja wilaya 12 zitakazofanyiwa tafiti ni Bunda, Serengeti, Bariadi, Busega, Sengerema, Misungwi, Geita, Chato, Muleba, Bukoba, Kishapu na Shinyanga.

Alisema tafiti zao zinaonesha kwa wale wagonjwa waliofika tu hospitalini kwao, lakini bado kuna wagonjwa wengi wapo majumbani.

Kwa upande wake, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Kikatoliki cha Afya (CUHAS), Dk Anthony Kapesa alisema lengo la utafiti wao ni kuangalia chanzo cha viashiria vya magonjwa hayo na wamelenga kuwapima wagon- jwa 7,700 wenye hayo magonjwa.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi