loader
Picha

Exim yazindua kampeni maalumu kwa wateja

BENKI ya Exim Tanzania imezindua kampeni maalumu, inayolenga kuhamasisha wateja wake kuhusu matumizi ya mtiririko wa huduma maalumu za ki- usalama, kwenye masuala ya fedha zinazotolewa na benki hiyo.

Kupitia mtiririko huo imebainishwa kuwa wateja wa benki hiyo, wanapata huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya usafirishaji wa fedha kwa usalama, huduma ya kiusalama ya malipo, huduma za kisasa za hundi na huduma ya kuweka pesa kwenye akaunti ya benki hiyo wakati wowote kwa kutu- mia mashine ya kuwekea fedha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Stanley Kafu alisema kupitia huduma hizo, wateja wa benki hiyo hawahitaji tena kupanga foleni kwenye matawi ya benki hiyo ili kupata huduma za kifedha.

Pia alisema wateja hao ka- mwe hawatohofia muda wa kufungwa kwa huduma za benki hiyo, kwa kuwa wanaweza ku- pata huduma wakiwa kwenye maeneo ya kazi.

“Huduma hizi ni sehemu ya mkakati wa benki ya Exim Tanzania kutoa huduma kwa wateja bila kubanwa na muda wa kazi au umbali wa kijiografia,’’ alisema Kafu Akifafanua kuhusu huduma ya usafirishaji wa fedha, Kafu alisema inamuondolea mteja hatari ya kuibiwa, kuvamiwa, kunyang’anywa pesa wakati anazitoa ofisini kwake kupeleka benki, kwa kuwa atapatiwa huduma ya kusafirisha fedha hizo kuelekea na kutoka benki kwa kutumia usafiri maalumu ukiwa na walinzi wenye mafunzo maalumu ya kulinda fedha.

“Kupitia huduma yetu ya Host to Host Srvice, mteja wetu anaruhusiwa kutumia matawi yetu yote Tanzania nzima kupokea malipo yake ya invoices kutoka kwa wateja wake wote nchi nzima.

Huduma hii ni kwa wateja ambao wanatoa na kupokea hundi nyingi kutoka kwa watu mbalimbali kama vile vyuo vikuu, shule, viwanda, kampuni za usafirishaji, kumpuni za clearing and forwarding, bisahara za mitandaoni, shughuli kama hoteli na utalii,’’ alisema.

Aidha, akizungumzia huduma ya ‘corporate cheque capture’, Kafu alisema huduma hiyo inayotumia ‘scanner’ inamwezesha mteja kuweka hundi zake wakati wowote bila kutembelea tawi lolote la benki.

“Hakuna haja ya kupanga foleni tena, huduma ipo ofisini au nyumbani kwako. Huduma hii ni maalumu kwa wateja wote wenye biashara ambazo zinapokea hundi kwa wingi kila siku bila kujali ni shilingi za Tanzania ama dola za Marekani, au inatoka benki gani hapa Tanzania.

Hapa tunahusisha biashara kama za usafirishaji, mashirika ya bima, wauza magari au pikipiki na vipuli, maduka ya jumla, mawakala wa gesi, pamoja na viwanda mbalimbali.’’ alisema.

Kuhusu huduma ya mashine ya kuweka fedha, alisema inamsaidia mteja kuweka pesa kwenye akaunti ya benki hiyo wakati wowote, bila kutembelea tawi la benki.

ILI kukabiliana na ugonjwa wa Covid- 19 unaosababishwa na virusi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi