loader
Picha

Serikali yashushia neema wajawazito, watoto

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen amesema Sh bilioni 5.5 zimepokelewa kutoka serikali kuu kwa ajili ya ukarabati na ujenzi mpya wa miundombinu ya kutolea huduma za dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (CeMONC) katika vituo vya afya 13.

Dk Kebwe alisema hayo mjini Ifakara jana katika taarifa yake kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa ziara yake mkoani Morogoro.

Mkuu wa mkoa alivitaja vituo vya afya vilivyopokea fedha hizo na halmashauri za wilaya zake katika mabano kuwa ni Mtimbira na Ngoheranga ( Malinyi), Kibati ( Mvomero), Mkuyuni , Mikese, Kinonko , Duthumi na Kisemu (Morogoro).

Vituo vingine vilivy- opata fedha hizo ni Gairo (Gairo),Mlimba na Mchombe ( Kilombero), Lupiro ( Ulanga), Kidodi, Mikumi na Malolo ( Kilosa) .

“Vituo hivi vyote ukiacha cha Malolo wilayani Kilosa, vimepokea fedha kutoka serikali kuu jumla ya Sh bilioni 5.5,” alisema Dk Kebwe.

Alisema hadi sasa vituo vya afya vya Kibati, Mtimbira, Kidodi , Mikumi , Gairo, Mlimba na Mang’ula wananchi wameshaanza kupata huduma kwenye majengo mapya .

Dk Kebwe alisema vituo vyote vitakapokamilika, mkoa utakuwa na vituo vya afya 25 venye uwezo wa kutoa huduma za dharura sawa na asilimia 48 ya vituo vyote vya afya vilivyopo mkoani humo.

“Lengo ni kufikia asilimia 70 ya vituo vyote vya afya vitakavyokuwepo vyenye uwezo wa kutoa huduma za upasuaji ifikapo Desemba mwakani, ”alisema.

Dk Kebwe alisema Sh bilioni 1.5 zimetolewa kwa kila mmoja, Wilaya ya Mvomero imepatiwa Sh milioni 500 na hivyo kufanya fedha iliyopokelewa kufikia Sh bilioni tano.

Akizungumzia usimamizi wa huduma za dawa, alisema mkoa unaendelea kufanya usimamizi na hali ya upati- kanaji wa dawa imeendelea kuimarika hadi kufikia asilimia 92.7 Juni, mwaka huu.

“Tunatoa shukrani za dhati kwa serikali kwa kutoa Sh bilioni 3.3 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa mwaka 2018/19,” alisema Dk Kebwe.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Kilombero

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi