loader
Picha

Moi atimiza miaka 95, awa kivutio kisiasa

RAIS wa zamani wa Kenya, Daniel Arap Moi mwezi huu amesherehekea kutimiza umri wa miaka 95 ya kuzaliwa kwake. Moi aliyeiongoza Kenya akiwa rais kuanzia mwaka 1978 baada ya kifo cha rais wa kwanza wa nchi hiyo, Mzee Jomo Kenyatta hadi mwaka 2002, alizaliwa Septemba 2, mwaka 1924.

Kabla ya kuwa rais, Moi ambaye kitaaluma ni mwalimu, alikuwa makamu wa rais wakati wa utawala wa Jomo Kenyatta kuanzia mwaka 1967 hadi mwaka 1978 aliporithi mikoba ya Mzee Kenyatta.

Kiongozi huyo ambaye ametimiza miaka 17 tangu aondoke madarakani, jina lake limerudi katika medani za siasa nchini Kenya kutokana na joto la uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2022.

Viongozi wote wa- naotarajia kuingia katika kinyang’anyiro cha ucha- guzi mwaka 2022 wanapigana vikumbo kufika nyumba- ni kwake wakiamini kuwa kukubaliwa na Mzee Moi ni sawa na kupata baraka zake na kuwa na uhakika wa kupata ushindi.

Waliomtembelea Mzee Moi mpaka sasa ni Rais Uhuru Kenyatta akifuatiwa na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga ambao wote walikwenda kumweleza Mzee kile walichokubaliana katika maridhiano yao yaliyotangazwa Machi 9 mwaka jana.

Viongozi waliofuata ni Naibu wa Rais, William Ruto aliyefika na kumweleza Mzee Moi nia yake ya kugombea urais mwaka 2022. Baada ya hapo walifuata viongozi wa ODM wakiongozwa na Hassan Joho.

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva ...

foto
Mwandishi: NAKURU

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi