loader
Picha

Ruto arudi tena ukanda wa Pwani

BAADA ya muda mrefu kupita bila kufika katika Kanda ya Pwani, Naibu Rais William Ruto ameamua kurudi tena katika eneo hilo ambalo ni ngome ya upinzani chini ya chama cha ODM, ikiwa ni kujiweka sawa katika uchaguzi wa mwaka 2022.

Lakini wachambuzi wanasema kinachomrudisha huko mara hii sio kuimaliza ngome ya upinzani kama alivyonuia katika ziara ya kwanza miezi mitano iliyopita, bali ni kuwahakikishia baadhi ya wanachama waliokuwa wa ODM lakini wakamuunga mkono kuwa bado ana nguvu na anastahili kuungwa mkono.

Baada ya ODM kuanza safisha safisha ya wanachama walioasi na kumuunga mkono Ruto, hofu imemkumba kiongozi huyo kuwa huenda wakampa mkono wa kwaheri wakiogopa kutupiwa virago.

Baadhi ya wanachama ambao wameonesha kuogopa kitisho la ODM ni pamoja na Mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa ambaye alijibatiza kuwa ni mfuasi kindakindaki wa Ruto ingawa ni mbunge kwa tiketi ya ODM.

Wachambuzi wengine wanaiona ziara hiyo ya Ruto kama jibu la Rais Uhuru Kenyatta ambaye alimaliza ziara katika kanda hiyo wiki iliyopita ambapo alitumia siku tano kutembelea kanda ya Pwani.

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva ...

foto
Mwandishi: NAIROBI

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi