loader
Picha

TAHLISO yaomba usalama vyuoni kuhimarishwa

JUMUIYA ya Wanafunzi wa Taasisi ya Elimu ya Juu(TAHLISO) wameiomba Serikali na vyuo nchini kuhimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi vyuoni ili waweze kutimiza wajibu wao wawapo vyuoni.

Aidha amewataka wanafunzi hao pia kuhakikisha wanasoma kwa bidii muda wote ili waweze kupata nafasi mbalimbali za kuliletea maendeleo Taifa lao katika siku za usoni na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuboresha viwango vya elimu.

Hayo yamebainishwa na na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Peter Niboye alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali ya shirikisho hilo zikiwemo ziara ya wajumbe wa TAHLISO waliyoifanya katika miradi ya kiserikali na taasisi mbalimbali ikiwemo Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) Akizungumzia hatua ya kuhimarishwa kwa usalama vyuo na wanafunzi vyuoni, Niboye alisema kuna haja kwa Serikali pamoja na uongozi wa vyuo kuhakikisha kunakuwepo na usalama dhidi ya masuala mbalimbali yanayowakabili wanafunzi na hivyo kuwafanya kuwa na hali ya mashaka.

Bila kuvibainisha madhara na vyuo vilivyowahi kukumbwa na taharuki ya ukosefu wa usalama, Niboye alisema kuwa kulingana na matukio na tabia mbalimbali za baadhi ya watu, kuna kila sababu ya kuhimarisha kwa usalama huo hatua ambayo pamoja na mambo mengine itawawezesha wanafunzi kutimiza malengo yao kwa amani wawapo vyuoni.

"Tunaamini Serikali ina mkono mrefu wa kubaini mambo mbalimbali ya kiusalama, hivyo ni vyema ikaendelea kushirikiana na vyuo hivyo na kuviangazia kwa karibu katika kusimamia suala la usalama wa wanafunzi ikizingatiwa ndani ya miezi michache ijayo vyuo hivi vinakwenda kufunguliwa" alisema Niboye.

Aidha aliwasihi wanafunzi Aidha akizungumzia ziara iliyofanywa na TAHLISO katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya NACTE, Niboye pamoja na kubainisha faida walizozipata kwa kuitembelea taasisi hiyo, alisema wao kama wadau ambata wa taasisi hiyo na zingine zikiwemo Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) pamoja na Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB), inawapa mwanya wa kuzitambua vizuri.

"Kupitia ziara yetu NACTE tumeweza kujifunza mambo mengin ikiwemo namna ya uombaji wa namba za utambuzi(AVN) pamoja kufahamu makosa wanayoyafanya wanafunzi wakati wa uombaji na mengineyo; tunawasihi wanafunzi kutembelea mara kwa mara NACTE pamoja na tovuti yake ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili" alisema Niboye.

Aidha alisisitiza kuwa ziara yao NACTE kwa kiasi kikubwa imeweza kuhimarisha ushirikiano wao huku akivitaka vyuo vyote nchini vilivyopo chini ya Baraza hilo kufuata kanuni na vigezo walivyoelekezwa ikiwa ni pamoja na kuzingatia mitaala ya ufundishaji kama ilivyoelekezwa ili kuzalisha wataalam bora.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi